Nothing Phone ni moja kati ya simu janja ambazo ziliingia katika soko na kushangaza wengi…wengi walikua wakishangazwa na muonekano wake wa nje.
Nothing Phone wao ni wageni kabisa katika soko la simu janja na baada ya simu yao ya kwanza kufanya vizuri sasa wako katika hatua za kulitoa toleo la pili la simu yao.
Ni wazi kwamba pamekua na vuguvugu kubwa la simu hii likiwa linaonyesha habari kadha wa kadha kuhusiana na simu hii katika mtandao.
Kupitia vyanzo rasmi vya kwao wenyewe, Nothing wametoa taarifa kwa umma kwamba tarehe 11 ya mwezi wa saba watapata kutambulisha simu yao hiyo mpya.
Nothing Phone (1) yenyewe iliachiwa rasmi mwaka 2022 ya mwezi wa saba ikiwa ni tarehe 21. Mpaka sasa kuna fununu nyingi katika mtandao zote zikiwa zinaelezea namna ya simu hii mpya itakavyokua.
Cha muhimu ni kwamba simu hii huwa ina muonekano pekee ambao haufananishwi na simu nyingine hivyo basi kampuni imesema kuwa imejitahidi katika kuhakikisha kuwa inazidi kuboresha muonekano huo kupitia simu hii inayokuja.
Nothing Phone (2) yenyewe itafanya uzinduzi wake huko marekani na kuifanya ni simu ya kwanza kuweza kufanya hivyo katika kampuni hiyo, kwa hiii hatua tuu inaonyesha ni jinsi gani ambavyo nguvu nyingi imewekezwa katika simu hii.
Wakati kampuni inasema kuwa imejitahidi sana katika kuhakikisha kuwa inaboresha kila kitu kuanzia muonekano, sifa za undani na ufanishi watumiaji wengi wa simu janja wana shauku ya kutaka kuona jinsi simu hiyo itakavyokuwa.
Pia kutakua na nguvu kubwa ambayo imewekwa ili kuhakikisha kuwa programu endeshi inaufanisi wa kutosha ukilinganisha na ile ambayo ilikua inapatikana katika Nothing Phone (1).
Mpaka sasa hakuna sifa za undani ambazo zimetolea licha ya fununu tuu, pindi sifa hizo zikiachiwa katika vyombo aminika basi TeknoKona itakujuza kama kawaida.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je ushawahi kutumia kifaa chochote kutoka katika kampuni hii? Niandikie hapo chini katika uwanja wa maoni.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.