Notisave ni app ambayo ina uwezo wa kufanya mambo mengi, lakini moja ya kitu muhimu sana unachoweza kuitumia app hii kufanikisha ni kuweza kudownload na kuhifadhi (save) WhatsApp Status za mtu yeyote bila yeye kufahamu.
Notisave ni app inayokuwezesha kupunguza idadi ya taarifa fupi (notifications) zinazotokea kwenye eneo la juu la simu yako, app hii inakuwa sehemu kuu ya wewe kuona notifications zote za apps mbalimbali.

Kupitia eneo la Chats la app hii utaweza kuona mjumuhisho wa taarifa fupi mbalimbali kutoka apps za kuchati kama vile WhatsApp na Messenger. Kwa upande wa WhatsApp ni eneo hili ndilo utakuta status zote zinazoonekana kwa sasa kwenye app ya WhatsApp.
Unaweza kutazama status hizo na pia kwenye status ya picha au video kwa chini utaona kuna eneo la kukuruhusu wewe kuweza kuhifadhi status (yaani picha/video) hiyo kwenye simu yako.
Nje ya hapo utaweza pia kusoma na kujibu jumbe/chats za apps kama vile Telegram, WhatsApp na Messenger moja kwa moja kupitia app hii badala ya kwenda kwenye app zenyewe.
Je umeweza kujaribu? Je unafahamu app nyingine inayokuwezesha kudownload status za WhatsApp kwa urahisi? Tuambie kwenye comment.
Download bure kupitia Google PlayStore/Notisave.