Katika mawasiliano ya kila siku kwenye simu janja WhatsApp inaweza kuwa kinara ya programu tumishi ambazo unazitumia sana na kwa sababu hiyo inawezekana kabisa vitu unavyovipokea vinajaza memori ya simu janja bila sababu ya msingi.
Kutokana na kutumia sababu ya kutumia WhatsApp kwa miaka mingi sasa vilevile nikiwa mpenzi wa masuala ya teknolojia na kupenda kutafuta njia mbadala wa matumizi ya kidijiti imesababisha kuwa mtu wa kutaka kujua zaidi namna bora ya kutumia programu tumishi nyingi tuu lakini leo hii nitazungumzia namna gani unaweza ukaokoa diski uhifadhi kujaa bila sababu ya msingi kutokana na WhatsApp.
Je, kwanini ni muhimu kuwa mwangalifu na matumizi ya memori kwenye simu?
Sababu ni kwamba watu wengi tunanunua simu janja amabazo zina memori ndogo (angalau GB 16) sasa ukipiga hesabu idadi ya programu tumishi ambazo utahitaji kuwa nazo kujumlisha na zile ambazo tayari zinakuwepo kwenye rununu unakuta zinakula nafasi ya karibu GB 2; kwa maana hiyo zitakuwa zimebaki GB 14 za diski uhifadhi kukubali kupakua masasisho ya programu tumishi, jumbe unazopokea, n.k hivyo ni muhimu kutafuta mbinu ya diski uhifadhi kutotumika kwa kiasi kikubwa.
Unapotumia WhatsApp kuna namna ya kufanya vitu ambavyo unavipokea (picha, picha za mnato) zisiweze kuchukua nafasi ndani ya simu; unakuwa unaviona lakini havihifadhi kwenye memori ya simu:
>Kuzuia kwa mtu/kundi mojamoja. Hapa unaweza kuchagua vitu anavyokutumia mtu/vinavyotumwa kwenye kundi fulani ndio visiingie kwenye diski uhifadhi je, unafanyaje? Ukiangalia taaria za mtu unayewasiliana nae kwenye WhatsApp utaona kipengele cha “Media visibility” kwenye Android au “Save to camera roll” kwa iPhone. Ukibofya hapo utaweza kuchagua vitu ambavyo unavipokea kutoka kwenye kundi/mtu husika vihifadhiwe kwenye simu au la!
Njia ya pili ni kuzuia kwa ujumla (watu/makundi yote). Ukiingia kweneye mpangilio (settings) ndani ya WhatsApp kisha ukaenda kwenye “Chats“>>”Media visibility” (Android) ama “Save to camera roll” ndani ya iPhone utaweza kuruhusu au kuzuia vitu vinavyotumwa kwenye kundi/ mtu kwa faragha visiweze kuhifadhiwa ndani ya memori ya simu.
Ukiona kama kuna picha ambayo ungependa uihifadhi kweye mfuko wa picha basi bofya kwa sekunde kadhaa picha husika kisha chagua “Save to gallery“.
Kama utakuwa unafuatilia mwenendo wa simu yako inajazwa sana picha za kila aina zikiwemo na zie zilizotumwa kupitia WhatsApp basi makala hii imekupa darasa la kutosha kuhusu mbinu ya kutumia kupunguza kujaza diski uhifadhi.
Vyanzo: TechniPages, mitandao mbalimbali
One Comment