OnePlus ni kampuni inayosifika kwa kuja na simu zenye sifa za kipekee sana, wanalenga kushindana na simu bora zaidi zilizo sokoni, na sasa wamekuja na kitu cha kitofauti. Kupitia OnePlus Ace 2 Pro wameleta teknolojia mpya, teknolojia ya kuwezesha kutumia simu yako ata kama mikono yako imelowa.
Kwa muda mrefu sasa huwa tunaepuka kutumia simu mikono yetu ikiwa imelowa kwani matone ya maji yamekuwa yakifanya display za simu kuhesabu miguso ambayo haipo, matone yakisababisha simu ichukulia ni kama miguso ya mtumiaji simu.
Teknolojia ya Rain Water Touch Control (Teknolojia ya udhibiti wa miguso ya maji ya mvua).
Teknolojia hii inawezesha simu hii kuweza kufanya kazi kama kawaida katika hali ya mvua, ikitumia teknolojia ya AI/algoriti maalum kuweza kutofautisha kati ya mguso wa makusudi wa mtumiaji simu dhidi ya ile miguso ya bahati mbaya inayosababishwa na matone ya mvua au majimaji. Hivyo kumuwezesha mtumiaji kuweza kutumia simu yake bila haja ya kukausha simu na mikono yake.
Teknolojia hii itawasaidia watu wanaojikuta kwenye hali ya kuhitaji msaada wakiwa kwenye hali mbaya za hali ya hewa, kama mvua, kwani kwa sasa mtu huyo atakuwa na changamoto ya kuhakikisha mikono yake na simu yake vyote visiwe vinaguswa na maji ili kumuwezesha kupiga simu bila makosa.
Nini kingine kizuri kuhusu OnePlus Ace 2 Pro?
Si teknolojia hiyo tuu, bali simu hii pia ni simu ya hadhi ya juu (Premium) kwa kuwa inakuja na sifa nzuri za kiteknolojia katika vipuri vyake.
- Prosesa: Snapdragon 8 Gen 2, hii ni prosesa ya kisasa na za hadhi ya juu kutoka Qualcomm. Zinautendaji wa hali ya juu zikiwezesha uchezaji wa magemu na apps nyingine nzito kwa ufanisi wa hali ya juu, pia ufanisi wake unasimamiwa na teknolojia ya AI ndani yake.
- Display/Kioo: Ukubwa wa inchi 6.74 OLED 1.5K, 120Hz, HDR10+
- Betri: mAh 5,000, teknolojia ya kuchaji ya kiwango cha 150 inayowezesha kuchaji simu hii ndani ya dakika 17 tuu.
- Kamera: Kamera 3, kuu ikiwa ya MP 50, MP 8 (ultrawide), MP 2 (Micro)
- RAM na diski uhifadhi: Kuna matoleo mawili, la RAM GB 16 na Diski ufidhai wa GB 256 au gb 512, la pili linakuja na RAM ya GB 24 huku diski uhifadhi ukiwa wa TB 1.
- Programu Endeshaji: Android 13.4 likiwa na muonekano spesheli kutoka OnePlus na Oppo la ColorOS.
Bei zitakuwa vipi?
Toleo (RAM + Disk Uhifadhi) | Bei – China | Makadirio kwa Dolla | Makadirio kwa Tsh |
16GB + 256GB | CNY 5,999 | USD 925 | TZS 2,312,500 |
16GB + 512GB | CNY 6,499 | USD 1,003 | TZS 2,507,500 |
24GB + 1TB | CNY 7,999 | USD 1,235 | TZS 3,087,500 |
*Kumbuka bei hizi za Tsh ni za kukupatia muongozo tuu, bei inaweza kuwa tofauti zikipatikana huku kutokana na sababu za biashara na kodi.
Je una mtazamo gani juu ya teknolojia hii kutoka OnePlus? Kumbuka hakuna simu janja nyingine yenye sifa kama hii kwa sasa kwenye simu zinazolenga watumiaji wa kawaida. Hapa OnePlus wamewapiku Apple na Samsung, je unadhani hii ni teknolojia muhimu kwako?
No Comment! Be the first one.