OnePlus wanazidi kujitanua na kwa sasa kampuni haijajikita katika kutengeneza na kuuza simu tuu bali wameongeza mambo mengi tuu ikiwemo TV, saa janja n.k.
OnePlus kwa kushirikiana na kampuni ya Keychron wana mpango wa kuleta katika soko keyboard ya kompyuta tena ile ni ya mfumo wa Keyboard.
Ukiachana na hili kampuni bado inasema kuwa itazidi kuongeza wigo wa bidhaa zake na haitaki ijulikane kwamba inatengeneza bidhaa fulani tuu.
Mpaka sasa keyboard hiyo haijajulikana jina lake na pia hata sifa zake za undani ambazo pengine inaitofautisha na keyboard zingine bado hazijawekwa wazi.
Siku ya keyboard hii kuachiwa bado haijajulikana kalini mwezi disemba tarehe 15, 2022 OnePlus imeweka wazi kuwa itatoa taarifa zaidi kuhusiana na swala hili.
Ukaichana na Keyboard bado kampuni inatarajia kuachia monitor zake mpya kabisa kwa mara ya kwanza kabisa nchini India na hii itakua ni disemba 12.
Ni wazi kuwa kampuni ina mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa inazidi kujitanua na kuwa na bidhaa nyingi chini ya wigo wake.
Ukiachana na hayo yote vile vile kampuni inakua kwa kasi sana na hii ni ukilinganisha na hapo mwanzo jinsi ilivyokua.
Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni ambayo imejulikana duniani katika swala zima la kutengeneza na kuuza simu kubadilika na kujitanua kuwa na bidhaa nyingi mfano mzuri Samsung.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je unadhani unaweza ukaanza kutumia keyboard hii? Je ni bidhaa gani ya OnePlus ushawahi kuitumia?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.