Watumiaji wa WhatsApp duniani kote wamekuwa hawana uwezo wa kuonyesha hisia zao kwenye jumbe wanazopokea na hivyo kuonekana kuna kitu fulani kinakosekana kwenye programu tumishi yenye watu wengi wanaoitumia kila siku.
Kuna raha ya kuwa mmiliki wa vitu vingi ambavyo unakuwa na uhuru navyo kwa asilimia zote. Tofauti ya WhatsApp na Facebook ipo na inaonekana waziwazi lakini pia kuna vitu ambavyo vipo upande mmoja na vinaletwa kwa nduguze. Ndio, watumiaji wa WhatsApp wapo mbioni kuja kuona kile ambacho wanaweza kukifanya kwenye Facebook Messenger ndani ya programu tumishi iliyotokea kupata wingi kubwa la wanaoitumia.
Inaelezwa kuwa baadhi ya watu waliopo kwenye kundi la kufanyia majaribio ya maboresho yanayofanywa na WhatsApp wamepata kuwa na uwezo wa kuonyesha hisia zao kwenye jumbe ambazo wanapokea. Yaani kama ilivyo kwenye Facebook Messenger mtu anapokutumia ujumbe una uwezo wa kuonyesha kupendezwa, huzuni, kucheka, n.k basi ndio hivyo hivyo kwenye WhatsApp.

Kwa sasa vitu hivi vizuri wenye kuviona ni wale tu walio kwenye orodha ya waliopewa idhini ya kujaribu vitu vipya kabla ya wengine na hii ikihusisha programu endeshi mbili-iOS na Android.
Ni matumani ya wengi kuwa maboresho hayo yataanza kupatikana kwa watu wote ndani ya siku za usoni.
Vyanzo: WaBetainfo, GSMArena
No Comment! Be the first one.