OpenAI, kampuni iliyounda ChatGPT, maarufu kwa uwezo wake wa kujibu maswali na kuunda maandishi, imechukua hatua kubwa kuelekea kwenye siku za usoni za teknolojia. Ushirikiano huu unalenga kuunda roboti zenye uwezo wa kujifunza na kuzoea mazingira mapya hivyo kufungua uwezekano mpya wa mwingiliano kati ya binadamu na mashine “kutusaidia katika maisha ya kila siku.” Lakini ni nini kinachofanya roboti hizi kuwa tofauti na zile ambazo tayari zipo?
Zaidi ya Automaton
Roboti nyingi za leo zinatumika katika viwanda, zikifanya kazi maalum na zilizoratibiwa kwa uangalifu. Robot za OpenAI zinatazamia kwenda zaidi ya hilo. Lengo lao ni kuunda roboti “zenye akili ya kutenda” (artificial general intelligence – AGI), maana yake ni kwamba zina uwezo wa kujifunza na kuzoea mazingira mapya, sio tu kufuata seti maalum ya maagizo. Fikiria robot inayoweza kukusaidia na kazi za nyumbani kama kupika au kusafisha, au hata kukusaidia na kazi za nje kama vile kuendesha mashamba au ujenzi.
OpenAI inajulikana kwa ujuzi wake katika maendeleo ya AI(Akili Mnemba), haswa katika uundaji wa lugha na kujifunza kwa kina. Kwa upande mwingine, Figure AI ina utaalamu katika uundaji wa vifaa vya roboti. Ushirikiano huu wa nguvu una uwezo wa kuziba pengo kati ya akili bandia na uwezo wa kimwili, na hivyo kuunda roboti zinazoweza kufanya kazi pamoja na wanadamu katika mazingira halisi.
Maadili na Usalama
Hata hivyo, maendeleo haya pia yanaleta maswali kuhusu maadili na usalama. OpenAI inasisitiza umuhimu wa kuendeleza AI kwa njia salama na yenye maadili. Watafanya kazi pamoja na Figure AI kuhakikisha kuwa roboti hizi zinatumika kwa manufaa ya binadamu na sio kinyume chake.
Iwapo OpenAI na Figure AI zitafanikiwa kuunda roboti hizi “zenye akili ya kutenda,” basi dunia inaweza kubadilika sana. Inaweza kumaanisha mabadiliko makubwa katika jinsi tunavyoishi na kufanya kazi. Endelea kufuatilia blogu yetu ili kupata habari zaidi kuhusu maendeleo haya ya kusisimua!
No Comment! Be the first one.