Makampuni mengi tuu ambayo yanajishughulisha na biashara ya bidhaa za kidjiti wana tabiti sokoni. Oppo nao wanaonekana wapo karibu tuu kujitosa kwenye biashara hiyo ambayo inawavutia wateja wengi sehemu nyingi duniani.
Ukiongelea Tecno, Samsung, Huawei na wengineo wote hawa wana tabiti toleo tofauti tofauti kwenye soko la ushindani. Katika habari zilizoibuka hivi karibuni inaonekana Oppo sasa wanaona ni wakati wao kuleta tabiti yao ya kwanza sokoni. Taarifa zinazoenea chimbuko lake likiwa kutoka huko Uchina kupitia mtandao wa Weibo inaonekana picha ya tabiti ikihusisha kampuni ya Oppo.
Tabiti hiyo ambayo inaaminika kuwa imetengenezwa na Oppo inafanana kwa karibu sna na MatePad Pro ya Huawei. Hii inatokana na kwamba muonekano wake na hata sifa zake ambazo zinaonekana kwa urahisi ni sawa na tabiti ya karibuni kabisa waliyoitoa Huawei.
Urefu wa kioo wa kwenye tabiti hiyo ya kwanza wanayotarajia kuja nayo Oppo ina urefu wa inchi 12.6. Mbali na hilo sehemu ilipo kamera ya mbele ni sawa kabisa na MatePad Pro.
Hii itakuwa ndio tabiti ya kwanza kutengenezwa na Oppo ambao wanaonekana wapo tayari kutoa na kuingia kwenye soko la tabiti ambalo lina wakongwe. Upo tayari kufahamu undani wa bidhaa hiyo mpya ya Oppo? Basi kaa nasi na tutakuhabarisha.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.