Oppo na OnePlus ni makampuni nguli kabisa katika teknolojia ya kutengeneza na kuuza simu japokuwa hayajaishia hapo, bado yana bidhaa kadha wa kadha za kiteknolojia
Kampuni hizi – Oppo na OnePlus —zilikumbwa na jambo baya na hii ni baada ya fununu kusambaa kwamba wanaachana kabisa na soko la ulaya.
Hii ni kwa maana kwamba simu hizo zitakua haziuziki kabisa katika masoko ya ulaya, hali ambayo ilileta taharuki kubwa kwa wateja wa huko.
Kingine ni kwamba fununu ilisema sio kwamba hili litatokea ulaya nzima na maeneo ambayo yataathirika ni Ujerumani, Uholanzi, Ufaransa na UK.
Ukiangalia ni kwamba masoko tajwa hapo juu ni masoko makubwa sana na ni vigumu sana kwa makampuni mengi kutaka kujitoa katika masoko hayo.
Fununu hizi zilipotokea tuu makampuni yote mawili yalizikanusha haraka sana kwa kutoa misimamo yao katika masoko hayo na kwa kifupi ni kwamba hawaondoki.
OnePlus
“OnePlus haiondoki katika siko la ulaya na itandelea kufanya biashara zake kama kawaida na vile vile itazididha uwekezaji ili kuahkiksisha unakuja na ubunifu wa hali ya juu na wa kisasa zaidi —Alisema bwana James Patterson, afisa mkuu wa masoko katika kampuni hiyo.
Oppo
“Mwaka 2023 tumeuanza vizuri sana katika bara la ulaya kwa kuzindua vifaa mbalimbali huku na tuna mpango wa kuleta vifaa vingine. Oppo itazidi kuleta vifaa vyenye ubunifu wa hali ya juu zaidi kwa ajili ya soko la ulaya – Alisema msemaji wa Oppo
Oppo Na OnePlus bado ni chapa zenye sifa kubwa sana katika soko, na vifaa vyake huwa vinauza sana na wapo katika kumi bora ya wauzaji wa simu kwa sasa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani makampuni haya yanahitaji sana haya masoko au hata wakiachana nayo wataweza kukua zaidi katika masoko mengine?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.