Kama wewe ni shabiki kindakindaki wa timu ya FC Barcelona ya nchini Uhispania, Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition inaweza ikawa simu nzuri kwa ajili yako.
Oppo, kampuni ya utengenezaji simu ya nchini Uchina imetengeneza simu ambayo ni maalumu kwa mashabiki wa timu hiyo ya FC Barcelona.
Muonekano wake nje na ndani umepambwa kwa rangi zinazotumiwa na timu hiyo Nyekundu na Buluu kuonesha uhalisia wa Barca ambao ni mabingwa wa La Liga.

Baadhi ya sifa za simu hiyo unaweza kuangalia hapo chini.
Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition.
Prosesa | Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 |
Network | GSM / CDMA / HSPA / EVDO / LTE |
Ukubwa wa Kioo | 6.6 inches (1080×2340) (AMOLED) |
Mfumo endeshi OS | Android 9.0 (Pie) |
Ukubwa wa uhifadhi | 128GB, 8GB RAM |
Kamera ya Nyuma | 48-megapixel (f/1.7) + 13-megapixel (f/3.0) + 8-megapixel (f/2.2) |
Kamera ya Selfie | 16-megapixel (f/2.0) |
ujazo wa Betri | Li-Po 4065 mAh (Haichomoki) |
Kampuni ya Oppo ambayo ni sehemu ya wadhamini wa timu ya FC Barcelona imeanza kuuza simu hiyo mwishoni mwa mwezi Julai katika nchi ya China, Spain, India, Holand, France na baadhi ya nchi za Ulaya.
Soma uchambuzi wa simu nyingine mbalimbali -> Teknokona/Uchambuzi