Kuna makampuni mengi ya simu ambayo yanafanya vizuri katika soko la nchini china lakini katika uuzaji wa simu za kujikunja Oppo wako kinara.
Ni wazi kuna simu nyingi za kujikunja (Fold) kwa sasa na makampuni mengi yameonekana yakikimbilia katika soko hilo huku Oppo nae akiwa hajabaki nyuma kabisa.
Sababu kubwa ni kwamba soko hilo linakua kwa kasi huku Samsung akiwa ametawala vikubwa katika soko la duniani.
Kampuni yenyewe imeona isiwe tabu na yenyewe imeamua kushikilia soko la china na taarifa hizi zimetolewa katika ripoti iliyoandaliwa na kampuni ya Canalys.
Ripoti hiyo inasema ni kwamba katika robo ya kwanza ya mwaka 2023 (Q1) kampuni ya Oppo ilitawala soko la nchini china kwa 31% ikiwa ni mbele ya makampuni mengine yote.
Lakini namba hiyo ni kwa simu za kujikunja tuu —ukaichana na simu janja za kawaida — huku namba hiyo ikiwa ni ongezeko kubwa maana kwa mwaka jana ilikua ni 12/ tuu.
Oppo Find N2 Flip imekua ni moja kati ya simu janja za kujikunja ambazo zinafanya vizuri katika soko hali ambayo ilipelekea Oppo kufanya vizuri katika sekta hiyo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani namba ya muazo ya simu za aina hii kutoka Oppo yatazidi kukua au yataporomoka na kuishusha kampuni?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.