App hii ya Outlook Lite ni mahususi kwa simu za Android ambazo zinatumia hazina uwezo mkubwa au zina matumizi madogo ya intaneti.
Wakati App hii, Outlook Lite imetangazwa kama iko njiani kuja tuliandika kuhusu jambo hilo >>HAPA<< hebu pitia tena.

Hapa hakuna kitu cha kushangaza sana kwani App hii ni kama App ile ya kawaida kabisa ya Outlook tuliyoizea tuu lakini hii ina ujazo mdogo na ni nyepesi Zaidi kulinganisha na ile tuliyoizoea.
App hii itakua ikiruhusu barua pepe (email) za akaunti Microsoft kama vile Outlook.com, Hotmail, Live,MSN, Microsoft 365 na hata Microsoft Exchange Online.
Ukiachana na hii ni kwamba App hii itakua haisapoti barua pepe zile za nje na mfumo wa Microsoft yaani kama vile Gmail na nyinginie nyingi.

Kizuri kuhisiana na App hii ni kwamba inafanya kazi vizuri sana hata katika simu zenyeuwezo wa 3G na 2G bila tatizo lolote
Kwa Sasa App Hii Inapatkana Katika Maeneo Ya.
- Argentina
- Brazil
- Chile
- Colombia
- Ecuador
- India
- Mexico
- Peru
- Saudi Arabia
- South Africa
- Taiwan
- Thailand
- Turkey
- Venezuela
Hapo mbeleni kuna uwezekano mkubwa wa huduma hii ya Outlook Lite kumfikia kila mtu duniani kote na kama inavyojulikana kwa sasa huduma hii inapatikana katika vifaa vya Android Pekee.

Outlook ni moja kati ya majukwaa makubwa kabisa katika maswala ya kutuma barua pepe na kupangilia vitu mbalimbali kwa kutumia kalenda.
Ningependa kusikia kutoka kwako, hebu niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unaweza kuwa unatumia huduma hii ?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.