Katika maadhimisho wa siku salama ya huduma ya intaneti duniani – Safer Internet Day, mtandao wa Google unawapatia watumiaji wake GB 2 zaidi za diski uhifadhi bure kabisa katika huduma ya Google Drive.
Safer Internet Day ni kitu ambacho inawezekana hujawahi kukisikia kabla ya leo, hii ni siku maalumu iliyoanzishwa kukumbushia watu umuhimu wa kuhakikisha akaunti zao zipo salama.
Katika kuhakikisha hilo linatokea Google wanawapa sababu za watu kuhakikisha wanapitia mipangilio (setting) za akaunti yao kuhakikisha kama mambo yote yapo sawa. NA MWISHO WANAKUPA ZAWADI YA GB 2 BURE KWENYE AKAUNTI YA GOOGLE DRIVE.
Promosheni ndio imeanza na inategemewa kuwepo kwa takribani wiki moja, inasemekana mwaka jana ilidumu kwa wiki moja.
Unaweza kwenda kuanza kuangalia taarifa muhimu za akaunti yako na kuhakikisha vitu kama vile sehemu ambazo akaunti yako ime-login n.k kupitia hapa -> Google Account Settings
Pia unaweza tembelea mtandao wa Safe Internet Day – https://www.saferinternetday.org/ ili kufahamu zaidi kuhusu siku huu, inaonekana maadhimisho yameshafanyika kwa takribani miaka miwili kwa sasa.
No Comment! Be the first one.