Kazi nyingi za siku hizi zinafanyika kwenye kompyuta hata hivyo, maisha yetu yanaonekana kuhamia kwenye simu janja. Wafanyakazi wenzetu, familia, jamaa na marafiki wanatupata kwa meseji, picha na sauti kwenye hizi simu.
Ingawa tunapenda tuendelee kufurahaia huduma hizi wakati wote, maisha inabidi yaendelee na ndiyo maana makala hii inakuletea njia rahisi ya kuunga simu na kompyuta ili maisha yako kazini yawe ya ufanisi zaidi.
Pushbullet ni app ndogo unayoweza kutumia kupata taarifa kutoka kwenye simu yako bila ya kuigusa. Inaweza kuwa muhimu kazini, unapohitaji umakini uwapo kwenye kompyuta. Pushbullet hutumia mfumo wa wayalesi na intaneti kukuonesha simu zinazoingia, sms zinazoingia, whatsapp na meseji nyingine za pupa kama Viber na BBM, alamu, muziki unaopiga na taarifa nyingine zinazotoka kwenye simu yako.
Unaanzaje kuitumia?
PushBullet inahitaji kuwa kwenye simu yako sambamba na kuwa kwenye kompyuta yako ili kufanya kazi yake.
- Pakua na pakia kutoka Play store ya Androidi na App-store kwa iPhone.
- Ingia kwenye wavuti www.pusbullet.com na pakua pushbullet kwenye Google Chrome na Mozilla au kwenye kompyuta za windows na mac.
- Kwenye simu yako, ingia kwenye Pushbullet > Bonyeza Menu > Settings > PC notifications. Ukiwezesha huu mpangilio, unaweza kutuma jaribio kwa kubofya ‘Send test notification’.
Pushbullet inategemea pia mpangilio kwenye ‘settings’ za simu yako unaoruhusu. Ingia kwenye Settings> Accessibility > Services na uiwezeshe PushBullet.
Mbali na kukupa taarifa, programu hii inakupa urahisi wa kujibu meseji zako punde zinapoingia, kutuma mafaili kati ya simu na kompyuta yako, simu nyingine na kwa watu wengine kupitia barua-pepe. Kama ziada, kuna uwezo pia wa kupata mishtusho (‘pushes’) kutoka vyanzo mbalimbali vya habari duniani.
Ki-msingi, pushbullet ni programu muhimu sana kwa wanaotumia kompyuta kuendesha mambo yanayohitaji umakini bila ya kukosa kujua kinachoita kwenye simu bila ya kuigusa. Unaweza pia kujifunza mengi kuhusu pushbulet kwenye tovuti yao ->> pushbullet na pia hzi video ->> pushbulet (youtube).
No Comment! Be the first one.