Kampuni ya Paypal inasaidia kukamilisha miamala katika mtandao yaani haina utofauti mkubwa sana na benki, kwa sasa imetangaza kuwa ina mpango wa kupunguza wafanyakazi wake.
Makampuni mengi ya teknolojia yamefikia uamuzi wa kupunguza wafanyakazi na mengi yaliaanza mara baada tuu ya janga la CORONA kuishambulia dunia.
Paypal wenyewe wanasema kwamba kazi hizi zitaathiri wafanya kazi 2,000 ambayo ni namba kubwa Sana kwa kampuni hiyo.
Upunguzwaji huo utafanyika katika wiki za hivi karibuni, namba hiyo ya wafanya kazi ambao watapunguzwa ni asilimia 7 ya wafanyakazi wote.
Rais wa kampuni hiyo, Bw. Dan Schulman amethibitisha taarifa hiyo na pia amewashukuru wafanyakazi ambao watapatwa na adha hiyo.
Sababu kubwa ambayo inapelekea mawazo haya ya kupunguza wafanyakazi ni sababu za kiuchumi ambazo zinaathiri sekta nyingi kwa sasa.
Baada ya kupunguza gharama kwa kuwapunguza wafanyakazi wake Paypal inategemea kupata pesa ya ziada $1.3 kwa mwaka 2023 pekee.
Pesa hiyo ambayo kampuni inaweza ikaamua kufanyia chochote kama vile kuiwekeza n.k . Japokuwa kampuni imeliweka hili wazi pia imeahidi kutobweteka na wako na mikakati ambayo itawepelekea kupata faida maradufu.
Paypal ilikua ikishuka kidogo kidogo katika soko la hisa, wameshuka sana kwa kipindi cha robo mwaka ya mwisho katika mwaka 2022.
Hali hii imewashangaza wengi na hata wawekezaji waliaanza kuhoji, hivyo hatua iliyofikiwa pia kwa namna moja au nyingine imechagizwa na jambo hili
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unahisi hii ni sawa? Kupunguza wafanyakazi ilimradi kampuni isonge?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.