iPhone 14 ikishatoka tuu, iPhone zingne zitaathirika hasa katika mauzo sio? Ukiachana na hayo bado simu hii inasubiriwa kwa hamu sana.
Japokuwa Apple wenyewe bado hawajaweka wazi jambo hili wenyewe, zinazosambaa sasa ni fununu tuu kwamba baadhi ya iPhone za nyuma zitaachwa kutengenezwa tena ili kupisha mauzo ya simu hizi mpya.
Ukifikiria ni kwamba mauzo ya iPhone 11 yanaweza yakamezwa kabisa na ujio wa iPhone SE 3 na kingine kikubwa ni kwamba iPhone 11 haina uwezo wa 5G wakati simu nyingi zinazotoka sasa hivi zina uwezo huo.
Kingine kikubwa ni kwamba ni vigumu sana simu za iPhone kukaa kwa miaka mitatu tangia zizinduliwe na kisha kuwa zinaendelea kuzalishwa tuu.
iPhone 12 Mini itauliwa na iPhone 14 Mini, hii ni kwa mujibu wa soko kuendana na iPhone 14 Max au hata toelo lile la Plus.
Kama unakumbuka vizuri nyuma iPhone 12 Mini haikupata mauzo mengi kama kampuni ilivyokua inategemea, hii pia inaweza ikawa ni sababu ya kampuni kuachana na simu hii katika uzalishaji.
iPhone 13 Pro na iPhone 13 Pro Max pengine nazo zitaachwa kuzalishwa, hapa unaweza ukawa una wasi wasi kidogo sio? —hahahaha, naelewa — lakini kitu cha msingi ni kwamba…
…kitu cha msingi ni kwamba tangia kampuni ianze kutoa matoleo ya Pro na Pro Max mwaka 2019, matoleo haya yajawahi kukaa zaidi ya mwaka.
Tusibiria mpka iPhone 14 itoke ili tuone mabadiliko …
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hii umeipokeaje? Je unadhani fununu hizi ni za kweli?
Kumbuka Kutembelea Mtandaoa Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.