Samsung ni kampuni kubwa sana ye teknolojia ambayo inajihusisha na mambo mengi kama vile simu janja, majokofu, runinga n.k na sasa inasemekana iko katika mpango wa kuja na saa janja yenye projector.
Projector ni vifaa vya kielektroniki ambayo tumevizoea hutoa picha/video katika kifaa husika na kuonyesha katika eneo lingine kama vile ukutani n.k na sasa Samsung inaripotiwa kuja na kifaa hiko.
Mpaka sasa kampuni ya Samsung ina saa janja na tayari zipo katika soko lakini ni kwamba saa hizo hazina projector.
Kingine ambacho taarifa hizi zinasema ni kwamba Projector hii sio ile ambayo inaweza kwenda ukutani kama tulivyozoea…
Hii ni kwamba itakua inaonyesha picha nyuma ya mkono, kwa kuona vizuri angalia katika picha ifuatayo
Kwa sasa kampuni ya Samsung imeshatuma maombi ya hakimiliki ya simu janja hiyo na kwa sasa jambo hili liko katika hatua za mwanzo.
Uzuri wa kifaa hiki ni kwamba kitakua na uwezo wa kunesha –katika mkono—taarifa ambayo ni tofauti na ile katika kioo cha saa hiyo na pia uwezo wa kuonesha hata video kadha wa kadha.
Sana sana hapa kinachofanyika ni kuongeza uwezo wa kuweza kuona katika eneo kubwa, na hili ni jambo zuri maana kuna baadhi ya muda unahitaji eneo kubwa tuu, pata picha hata ukiwa unafanya mazoezi.
Mpaka sasa hakuna taarifa za undani kabisa kuhusiana na jambo hili, na wengi wetu tunapenda tungeona hata video ya kifaa hichi ili kuiona vizuri na vile vile kujua sifa zake za undani.

Kingine ni kwamba kwa kupitia teknolojia hii basi unaweza ukashangaa ni saa janja zijazo zikawa hazina kioo (au kuwa na kioo kidogo) ili kuwa na projector.
Kingine ni kwamba hatuna budi kusubiri mpaka tuone Samsung wenyewe kuja kututangazia wenyewe kifaa hiki, na vile vile bado haiko wazi ni lini kitatoka.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika uwanja wa comment, je uko tayari kutumia saa janja ambayo ina projector?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.