Vivo ni moja kati ya Makampuni makubwa sana katika maswala mazima ya kiteknolojia na kwa sasa kuna swala ambalo linaikumba kampuni hiyo kutoka katika kampuni nyingine nguli ya Nokia.
Soko ambalo kampuni ya Vivo inaweza kulikosa huko ulaya ni lile la ujerumani ambalo ni moja kati ya masoko makubwa sana katika maswala mazima ya kuuza simu janja.
Unaweza ukawa unajiuliza mpaka sasa wawili hao wana jambo gani ambalo linapelekea yote haya, jibu ni rahisi sana maana ni maswala mazima ya hatimiliki baina ya kampuni zote hizo mbili.
“Vivo inaheshimu sana miliki za kiteknolojia na imejikita katika kuhakikisha kuwa inaendelea kufanya uchunguzi wa kina na kuja na ubunifu wa hali ya juu katika kuhakikisha kuwa kampuni inasonga mbele kwa kuwaletea wateja kile kilicho bora’’
Ukiachana na hilo ni kwamba Vivo imeingia katika mikataba mingi na makampuni mengine mengi katika maswala mazima ya kutoa leseni na kwa sasa wameongea/wamejadiliana na kampuni ya Nokia katika kuhakikisha kwa wanaongeza mkataba.
Katika maongezi hayo kampuni ya Nokia wameonekana kwa namna moja au nyingine haijafikia makubaliano na kampuni ya Vivo na hii ni hali hatarishi kwa kampuni la Vivo.
Kama muafaka usipofikiwa hii ina maana kuwa kampuni ya Vivo itasitisha huduma zote zinazohusiana na matangazo na manunuzi nchini ujerumani.
Kumbuka kwa makampuni ni jambo la kawaida sana kuwa wanachukua na vifaa/vipuri vya simu zao kwa makampuni mengine na hii inakua ni kwa mikataba maalumu baina yao ambayo wanaweza kuingia na kutoka.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani kampuni hizi mbili zitafikia muafaka juu ya jambo hili au ndio kampuni ya Vivo itaachana na soko hilo la ujerumani?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.