Masisho ya App yamekua ni mengi sana siku hizi na WhatsApp wanazidi kuushangaza ulimwengu kwa kuzidi kuongeza vipengele na kuboresha huduma yake.
Kwa upande wa ujumbe imekua ni jambo la kawaida maana tayari kipengele cha ujumbe wa kupotea kipo katika App ya WhatsApp na sasa ni zamu ya picha na video.
Hii inafanya kazi kwa kuhakikisha kabisa kwamba una toleo la juu (jipya) kabisa la WhatsApp ndio utaweza fanikisha hili.
Kinachofanyika hapa ni kwamba wakati unachagua video au picha za kumtumia mtu (ukishazipata) pembeni ya alama ya kutuma kuna eneo ambalo linaonyesha alama ya sekunde.
Mpaka sasa huduma hii inapatikana katika toleo la beta la namba 2.21.14.3. Hii ni kwamba baada ya toleo hili baadae inawezekana likaanza kupatikana katika toleo la kawaida la android
Lingine ni kwamba picha na video zinazotumwa kwa aina hii ni kwamba zitakuwa zinaagaliwa mara moja tuu na baada ya hapo zitapotea na hazitaweza kutizamwa tena.
Najua unaweza ukawa unajiuliza kwamba je unaweza kurekodi uso wa screen kama ukitumia picha na video za kupotea ili pindi zikifutika wewe bado uwe nazo.
WhatsApp haijaja na muarobaini juu ya hilo pia maana kamaa utapiga ‘screen shot’ au umerekodi uso wa video iliyotumwa kwa mfumo huu basi mtumaji hatapewa ujumbe wa taarifa kwamba umefanya hivyo kama mitandao mingine mfano Snapchat
Kwa kusema haya inabidi kuwa na uhakika au kuwa na tahadhari wakati unatumia kipengele hichi katika kifaa chako.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, hii umeipokea vipi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Katika Maswala Ya Sayansi Na Teknolojia Wa TeknoKona.Com. Kumbuka Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
No Comment! Be the first one.