Nakala ya mauzo milioni 30 ni nyingi sana kwa kifaa cha kielektroniki, Playstation ni moja kati ya makampuni makubwa kabisa ambayo yanamilikiwa na kampuni ya Sony.
Playstation 5 ilipofikisha mauzo ya nakala milioni 25 tulikuandikia >>HAPA<< na huu ulikua ni mwezi novemba mwaka 2022. Ukiachana na haya yote kampuni bado inakiri kuwa kampuni haijauza nakala nyingi kama ilivyokua inategemea.
Mwezi disemba mwaka 2022 ndio mwezi ambao umeibuka kidedea kama mwezi ambao umekusanya mauzo mengi ya kifaa hicho pengine kwa sababu ni mwezi wenye sikuku na wengi wanutumia kama sehemu ya mapumziko vile vile kupeana na kupokea zawadi.
Kampuni imewashukuru wateja wake ambao mara kwa mara walikua wakivumilia maana PS5 ilikua haijitoshelezi maana uhitaji ulikua mkubwa hali ambayo ilisababisha mpaka bei kupanda katika baadhi ya masoko soma zaidi >>HAPA<<
Ni wazi kwamba tangia mwezi novemba Sony ilianza kupata tabu katika kuhakikisha kuwa kinafikia uhitaji wa wateja wake wote wanaotaka kifaa cha PS5 sababu kubwa ikiwa ni changamoto katika uzalishaji.
Kingine kizuri kwa mwaka 2023 ni kwamba kampuni ina mpango wa kuja na toleo lingine la PS5 ambalo ni Playstation Slim na vile vile itakuja na Playstation VR2, soma zaidi >>HAPA<<
Ni wazi kwamba kampuni inazidi kufanya vizuri na linajitahidi katika kuhakikisha kuwa bidhaa yake inawafikia wateja wengi kadri inavyowezekana.
Kwa muda mrefu sana vifaa hivi vimekua vikitamba na kutawala kabisa katika soko la magemu huku kifaa hiki kikiwaacha mbali sana wapinzania wake mfano Xbox na wengine wengi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hili umelipokeaje? Je unadhani kampuni itaendelea kuuza nakala nyingi zaidi na pengine kuvunja rekodi ya Playstation 4?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.