Repeat.gg ni mtandao maarufu sana ambao unaendesha mashindano ya kimtandao mbali mbali kwa kutumia magemu kadha wa kadha.
Pengine ni moja kati ya mtandao mkubwa kabisa, kumbuka Playstation ilisema bado itanunua makampuni mengi sana na hata sisi TeknoKona tuliandika kuhusu habari hiyo na unununzi wake wa makampuni mengine, soma >>HAPA<<
Soma Zaidi kuhusiana na habari zote zinazohusu Playstation >>HAPA<<
Kitu ambacho hukijui kuhusiana na Repeat.gg ni kwamba, hili ni jukwaa kubwa sana na linahusisha wachezaji kuweza kushindania vitu mbalimbali ikiwemo hata pesa taslim n.k.
Kingine ni kwamba ili kushiriki katika michezo ya jukwaa hilo sio lazima uwe katika mtandao (online) kwa wakati husika
Yaani hii inamaana kuwa inawaruhusu wachezaji kushindana hata kama hawapo mtandaoni kwa wakati mmoja, hapa kinachofanyika ni kwamba teknolojia ya ulandanishi (synchronization) inahusika.
Kingine ni kwamba kampuni ina uwezo wa kutunza taarifa za wachezaji na alama zao za ushindi ili kulinganisha na kupata mshindi wa mashindano mbali mbali.
Playstation wanafanya ununuzi huu ili kujihakikishia ukuaji mkubwa katika Nyanja ya magemu, licha ya kuwa tayari wameshakua.
Ukichana na ununuzi huu bado Repeat.gg itakua inaruhusu utumikaji kwa michezo katika vifaa vyote yaaani kompyuta, simu janja, na vifaa vingine kama vile Plsyastation na vile vinavyofanana.
Ningependa kusikia kutoka kwako, hebu niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani Playstation iishie hapo katika kununua makampuni yananyojihusisha na magemu aua iishie hapo tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.