Polisi Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuweza kukabiliana na wale ambao wanabainika kutumia vibaya mitandao ya kijamii.
Kundi hilo ambalo lina jukumu la usalama wa raia na mali zake imeweka wazi mpango wake wa kuwasaka viongozi wa makundi ya WhatsApp ambao wanaendesha mtandao huo kwa mambo yasiyofaa.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa inasema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kuwabaini wale wote wanaoendesha biashara ya kujiuza na kuweka picha za uchi kwenye mitandao ya kijamii hususani kwenye Whatsapp na Instagram.