Hizi ndio programu muhimu za kuwa nazo kwenye kompyuta/ laptop yako inayotumia Windows 10. Iwe ni kwenye kompyuta yako mpya au ambayo ndio umeweka Windows 10 upya, tutakutajia programu muhimu pamoja na kuweka eneo la wewe kuzipakua/download.
Soma uchambuzi na kuhusu programu mbalimbali nyingine hapa – Teknokona/ Programu za Kompyuta
1. Kivinjari: Google Chrome
Bado Google Chrome ni kivinjari namba moja duniani. Uwezo wa kuhama na kuweka kumbukumbu za data zako hasa hasa password/nywila kwa urahisi ni moja ya faida ya kutumia kivinjari hichi.
Pia unaweza kuwezesha mambo mengi mengine kwa kutumia ‘extensions’ zinazopatikana katika soko la Chrome Extensions.
Ila pia kama unapendelea Firefox au Opera zaidi basi links zake hizi hapa chini.
Download: Google Chrome (Free)
Download: Firefox (Free)
Download: Opera (Free)
2. Programu ya Office: LibreOffice
Programu ya kuwezesha uchapishaji na usomaji wa document ni moja ya programu muhimu zaidi kuwa nayo kwenye kompyuta yako. Lakini je unafahamu ya kwamba sio lazima utumie Microsoft Office? Kuna programu inayopatikana bila malipo na ambayo pia inaweza kufanya yote unayoweza kufanya kwenye Microsoft Office.
Kuna maeneo ambayo unaweza kufanya mengi zaidii kwenye LibreOffice kuliko ata ambavyo ungeweza kwa kutumia Microsoft Office, mfano kwenye utumiaji wa mafaili ya PDF.
Soma uchambuzi wetu hapa – Mibadala Ya Bure Kwa Microsoft Office!
Download: LibreOffice
3. Programu ya Kucheza Video: VLC
VLC ni moja ya programu nyepesi na iliyobora zaidi katika utumiaji wa mafaili ya video. Hakuna video ambazo VLC itapata shida kufungua.
Je unafahamu ya kwamba unaweza pia kudownload subtitles za muvi kupitia VLC? Soma hapa
Download: VLC (Bure)
4. Muziki: MusicBee
Kwa wale wapenzi wa kusikiliza muziki kupitia kompyuta zao basi hakuna programu nzuri kwa ajili ya upangiliaji wa muziki, playlist na mengine mengi kama hii ya MusicBee – labda ipo ila bado sijakutana nayo.
MusicBee ni programu ya bure yenye uwezo mzuri wa kusoma mafaili yako ya muziki na kukupa uwezo wa kusikiliza kulingana na aina za nyimbo, wasanii, n.k.
Pia inakuja na eneo la Auto DJ, yaani unaweza kuchagua aina za nyimbo au msanii na baada ya hapo programu hii itakupangilia nyimbo yenyewe. Hii ni programu nzuri kwa watu wenye mafaili mengi ya muziki/nyimbo.
Download: MusicBee (Bure)
5. Programu ya Antivirus / Malware
Kwenye programu ya kukulinda dhidi ya virusi vya kompyuta huna uhitaji wa kudownload nyingine bali tumia Windows Defender ambayo inakuja moja kwa moja katika Windows 10. Hakikisha unaipatia masasisho ya mara kwa mara.
Ila siku hizi virusi sio tatizo pekee katika usalama wa kompyuta zetu hasa hasa tunaotumia huduma za intaneti sana kwenye kompyuta hizo. Hapa hakikisha unapata programu inayoenda kwa jina la Malwarebytes.
Hii ni programu ya usalama inayosaidia kukulinda dhidi ya viprogramu vya udukuzi vinavyokwenda kwa jina la ‘malware’, hizi zinapatikana sana kwenye huduma za mitandao na zikiingia kwenye kompyuta yake basi unaweza jikuta unapoteza mafaili yako au utaanza kuona matangazo hovyo sehemu zisizotakiwa kuwa na matangazo.
Download: Malwarebytes (Ingawa huwa inauzwa ila pia kuna toleo la bure ambalo linatosha)
6. Utumaji wa mafaili na kufungua mafaili: 7-Zip
Ingawa Windows 10 inakuja na uwezo wa kufungua mafaili yaliyohifadhiwa kwenye mfumo wa zip ila kwa kuwa na 7-Zip utapata uwezo wa kuweza kufungua na kufunga mafaili katika mifumo mingi zaidi kama RAR n.k.
Download: 7-Zip (Bure)
Hizi ndio programu 6 muhimu sana za kuhakikisha kompyuta yako ya Windows 10 ipo tayari kwa matumizi na kazi mbalimbali.
Je kwako ni programu gani nyingine muhimu sana unadhani tumeisahau hapa na ingestahili kuwepo hapa?