Programu ya Microsoft Office 2024 yaanza kupatikana kwa watumiaji wa programu endeshaji za Windows na MacOS. Toleo hili jipya linapatikana kupitia leseni ya ununuzi wa mara moja, hii ni tofauti na mfumo mwingine wa kupata programu za Office ya malipo ya kila mwezi – Microsoft 365.
Vipengele Muhimu vya Microsoft Office 2024
- Programu Zilizoboreshwa: Office 2024 inajumuisha matoleo mapya ya Word, Excel, PowerPoint, OneNote, na Outlook. Programu hizi zimeboreshwa kuendana na mahitaji mapya na huku usalama dhidi ya udukuzi ukiboreshwa zaidi kuendana na hali ya sasa. Mfano programu hizo zitaweza kufanya kazi kwa wepesi zaidi – kuweza kuhimili uwezo wa kufungua mafaili mengi kwa wakati mmoja bila kutumia kiwango kingi cha RAM ya kompyuta yako.
- Hakuna Usajili Unahitajika: Tofauti na Microsoft 365, Office 2024 inapatikana kwa ununuzi wa mara moja. Hii inamaanisha kuwa watumiaji hawatalazimika kulipa ada za kila mwezi au kila mwaka.
- Windows na macOS: Office 2024 inapatikana kwa mifumo yote miwili ya uendeshaji, ikiwapa watumiaji uhuru wa kuchagua mfumo wanaopendelea.
- Msaada wa Miaka Mitano: Microsoft itatoa masasisho na msaada kwa Office 2024 kwa kipindi cha miaka mitano, kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata huduma bora na za kisasa zaidi.
Faida za Office 2024
- Gharama Nafuu: Kwa kuwa ni ununuzi wa mara moja, watumiaji wanaweza kuokoa pesa kwa muda mrefu ikilinganishwa na usajili wa kila mwezi au kila mwaka.
- Usalama na Utendaji Bora: Programu zimeboreshwa ili kutoa usalama wa hali ya juu na utendaji bora, kuhakikisha kuwa data ya watumiaji inalindwa.
- Urahisi wa Matumizi: Watumiaji wanaweza kufurahia urahisi wa kutumia programu za ofisi bila kuwa na wasiwasi kuhusu ada za usajili.
Kwa ujumla, uzinduzi wa Microsoft Office 2024 ni hatua kubwa kwa watumiaji wanaotafuta suluhisho la kudumu na la gharama nafuu kwa mahitaji yao ya ofisi.
Bei: Office Home 2024, kwa matumizi binafsi ni $149.99 (Takribani Tsh 400,000/=) na inakuja na programu za Word, Excel, PowerPoint, na OneNote, leseni ni ya kwa kompyuta moja tuu. Toleo la Office Business bei rasmi ni $249.99 (Takribani Tsh 680,000/=) na linakuja na programu zote za Office Home, pamoja na programu ya Outlook. Kumbuka bei zinaweza zikawa juu zaidi nchini kutokana na gharama za kikodi.
No Comment! Be the first one.