Kampuni nguri katika utengenezaji wa magari ya Toyota wametambulisha rasmi kifaa ambacho wamekuwa wakikifanyia kazi kwa muda sasa kwa ajili ya kuwasaidia watu wasioona (vipofu) katika kuweza kutembea bila msaada.
Kwa miaka mingi watu wenye matatizo ya kuona wanaitaji vitu kama fimbo, mbwa n.k katika kuwasaidia kutembea. Toyota wametambulisha rasmi mradi walioupa jina la ‘Project BLAID’ ambapo wanategemea kuweza kuanza kufanyia majiribio kifaa hicho hivi karibuni.
Kifaa hicho ambacho kitavaliwa na mtu eneo la mabega kitaweza kumuelekeza mtu na kumtaarifu kuhusu vitu vilivyokatika eneo lake. Mfano kama ni gari, ukuta n.k.
Inategemewa mvaaji atapata taarifa zitakazoweza kumsaidia kutembea ndani maeneo kama vile maofisini na ata kwenye maduka makubwa (malls) huku kifaa hicho kikiweza kumpa taarifa juu ya vitu kama vile – choo, ngazi, milango n.k.
Kifaa hicho ndani yake kinakuja na kamera kadhaa kwa ajili ya kuweza kusoma mazingira, pamoja na spika kwa ajili ya kumpatia mvaaji taarifa kuhusu mazingira yake.
Toyota wanasema wanazidi kuifanyia teknolojia hiyo maboresho ili kuweza kuongezea kifaa hicho uwezo wa kutambua sura na vitu vingine mbalimbali (facial recognition & object identification).
Tayari Toyota wamepata sifa sana kutokana na juhudi zao katika project hii. Wenyewe wanadai ni jambo ambalo wameamua kulifanya kama juhudi zao katika kuleta maana zaidi ya msemo wao wa kibiashara wa “Lets Go Places” – yaani ‘Twendeni Sehemu/Pahali’ hili likimaanisha kupitia utumiaji wa magari yao ya Toyota.
Video kutoka Toyota kuhusu Project BLAID;
Kifaa cha “BLAID” Kitaanza kupatikana lini?
Kwa sasa bado wanafanya maboresho, na muda mrefu wataanza kufanya majaribio ya awali (beta testing)..hivyo bado ni mapema kusema ni lini kifaa hicho kitaingia sokoni na kuna uwezekano ata jina likabadilika.