Rais Paul Kagame wa Rwanda amezindua gari la kwanza aina ya Volkswagen lililounganishwa kwenye kiwanda cha Volkswagen kilichopo Kigali-Rwanda.
Gari hilo aina ya Polo ni la kwanza kuunganishwa katika kiwanda hicho huku kampuni hiyo ya magari ya Ujerumani ikitarajiwa kuunganisha vipuri vya magari 5,000 katika awamu ya kwanza ambayo kati yake yatakuwa ni magari aina ya Passat, Tiguan, Amarok na Teramont.
Rais Kagame akiwa katika uzinduzi wa gari aina ya VW lililounganishwa nchini kwake.
Kampuni ya magari ya Volkswagen ambayo ndio kubwa zaidi barani Ulaya, imefanya uwekezaji wa $20m (£15m) nchini Rwanda na ikitarajiwa kuajiri watu 1,000.
Kampuni hiyo inapanga kuuza magari hayo mbali na kuyatumia kama usafiri wa kukodi (taxi) ambapo wateja watawasilisha maombi ya kutaka huduma hiyo kupitia simu zao.
Uunganishwaji wa magari ukiendelea
Kuna takribani magari 200,000 ya watu binafsi yaliosajiliwa katika taifa hilo lenye zaidi ya watu milioni 12 kulingana na halmashauri ya kutoza ushuru nchini humo. Kampuni hiyo ya Ujerumani inapanga kupanua uwekezaji wake katika eneo la jangwa la Sahara baada ya kufungua kiwanda chake nchini Kenya 2016.
rais kagame akiendesha gari lililotengenezwa Rwanda
Wengine hawaamini kwamba magari ya Ujerumani yanaweza kuunganishwa nchini Rwanda, na leo tayari magari ya kwanza yamezinduliwa. Kiwanda hiki ni mwamko mpya katika safari ya Rwanda ya ukuwaji wa kiuchumi~Paul Kagame
Hata hivyo, $15,000 ambalo ndio gari (VW) la thamani ya chini zaidi; ni wazi kwamba magari hayo yatakuwa ghali mno kwa raia wengi nchini Rwanda.
Volkswagen tayari imejikita katika baadhi ya nchi barani Afrika, ambazo ni pamoja na Nigeria, Afrika Kusini na Kenya.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.