Kampuni ya Realme inamilikiwa na kampuni moja ambayo inamiliki simu za Vivo na Oppo ambayo inajulikana kwa jina la BBK Electronics
Kampuni hii ni kubwa na ina chapa nyingi ambazo zinajihusisha moja kwa moja na bidhaa za kiteknolojia na nyingi zinafanya vizuri.
Simu za Realme zimetangazwa kufikia malengo yake makubwa na hii ni baada ya kuvunja rekodi ya kuuza simu janja zake milioni 200.
Kampuni imeanzishwa chini ya miaka mitano iliyopita na inasema imesafirisha nchi nyingi simu zake hizo na nyingi ikiwa ni nje ya china.
Kwa chapa ya simu ambayo haijasambaa duniani kote inaonekana moja kwa moja namba hiyo ni kubwa sana na kama wakiendelea hivyo watafika mbali sana.
Mpaka kufikia mauzo ya simu milioni 200 ni kampuni chache sana ambazo zimefikia namba hiyo kwa uharaka sana nazo ni Vivo, Huawei, Samsung na Apple.
Kwa dunia nzima ni makampuni 14 tuu ambayo yameweza kusambaza simu duniani ambazo zinafikia idadi ya milioni 200
Kingine ni kwamba chapa (brand) za simu zimepungua sana maana nyingi zimetoka kabisa katika soko.
Kumbuka kwa mwaka 2017 kulikua na chapa 700 za simu lakini zilikuja kushuka mpaka kufikia 250 tuu mwezi septemba ya mwaka huu.
Wao Realme kwa sasa wanasema wana mpango wa kuja na simu kali zenye sifa za juu kabisa ili kuweza kuleta ushindani mkubwa katika soko.
Hii ni namba kubwa sana kwao Realme na inabidi wakaze sana buti kwa simu zao zijazo. Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.