Regina Duncan aliyekuwa mtendaji mkuu wa kitengo kimoja cha uvumbuzi cha Google ameondoka na kwenda kujiunga na kitengo kama hicho Facebook, Mbeijing huyo ambaye muda wake wa hapo Google umekuwa wa mafanikio makubwa anaenda kujiunga na kitengo pia cha uvumbuzi katika kampuni ya Facebook.
Regina Duncan anasifiwa kwa kuwa akiwa Google alifanikiwa kuongoza miradi mbalimbali ya kibunifu na ikafanikiwa, miradi aliyoiongoza mwana mama huyo ni pamoja na ule wa kutengeneza tatoo ya kidigitali na pia miradi miwili iliyo kuwa inatengeneza simu janja.
Katika makampuni makubwa sio jambo geni kwa kuajiri wafanyakazi ambao walikuwa katika kampuni ambayo ni mpinzani wako ila ni ukweli usiofichika kwamba Google imempoteza mtu ambaye alikuwa na mafanikio katika kazi alizofanya.
Facebook wamempata mtu muhimu hasa katika kipindi ambacho mtandao huu unayo miradi mingi ambayo inayohitaji kiongozi ambaye ana jicho na mtazamo wa ki bunifu kama Regina Duncan.
Akiwa facebook ataongoza kitengo ambacho kinaitwa Biulding 8 na alipo ulizwa kuhusu kuhama Google mwana mama huyo amesema kwamba hii ni nafasi yake kufanya kile kitu alikuwa anatamani kufanya siku nyingi na anahuzunika saana kuondoka Google. kwa upande wao Google wanasema kwamba wanamtakia kila la kheri mfanyakazi wao huyo wa zamani katika majukumu yake mapya.
Makala hii imeandikwa kwa msaada wa Mtandao wa PC WORLD na pia kwa msaada wa vyanzo vingine mtandaoni.