Moja katika ya masoko muhimu sana na yenye hela nyingi katika teknolojia ni soko la magemu. Toleo lililoboreshwa la Resident Evil 4 (Remake) lenyewe limejikuta likivinja rekodi ya mauzo.
Ni wazi kwamba yameshakuwepo matoleo mengi sana ya Resident Evil lakini toleo hili ndio linashikilia rekodi ya kuuza sana ndani ya kipindi cha masaa 48 tuu.
Kampuni ambayo inamiliki gemu hilo Capcom, wao wanatabiri kwamba jinsi mauzo ya gemu hilo yanvyoenda kwa kasi pengine wanahisi kabisa itakuaja kuvunja rekodi nyingine ya kuwa na mauzo makubwa katika magemu hayo.
Unaambiwa kwa muda wa masaa 48 (siku mbili) tuu gemu hiyo imeuza nakala zaidi ya milioni 3 na vifaa Gemu hii inatumika katika vifaa vya PlayStation 4, PlayStation 5, Xbox Series X|S, na kompyuta.
Mpaka sasa matoleo yote ya Resident Evil yameuza nakala zaidia ya milioni 135 duniani kote na kwa jinsi hali hii inavyokwenda ni kwamba namba hii itapanda sana muda si mrefu.
Kingine kinachowashangaza watu ni kwamba toleo hilo sio jipya kabisa bali ni mboresho tuu wa toleo la nyuma lakini mapokezi yake yamekua makubwa sana.
Kingine cha kukumbukwa hapa ni kwamba kwa Resident Evil 4 (ya kwanza) kabisa ilitoka mwaka 2005 na hivyo basi huu ulikua ni mboresho wa toleo hilo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la commen, je unahisi kwa hali hii ni kwamba na makampuni mengine yaanze kurudia upya matoleo ya magemu mengine?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.