Kama unatumia simu janja, Samsung Galaxy S7 unatakiwa ujihadhari na udukuzi kwani watafiti kutoka chuo kikuu cha Graz nchini Austria wamebaini kuwa simu hiyo ipo katika hatari ya kuweza kudukuliwa.
Siku si nyingi wanaomiliki simu janja hiyo walitahadharishwa kuwa simu zao zinaweza kudukuliwa kutokana na udhaifu uliobainika kitu ambacho mdukuzi anaweza akaingia kwenye simu hiyo na kujua vyote vilivyopo kwenye simu.
Tatizo hilo kwa lugha Kiingereza tunasema meltdown na kimsingi ni tatizo ambalo lilianza kuonekana kwenye vipuri vya Intel kwamba mdukuzi anakuwa na uwezo wa kuchungulia kwenye kipuri hicho na kuweza kuona taarifa.
Samsung waliweza kupewa taarifa na tangu hapo wamekuwa wakitoa masasisho ya kuifanya simu zote za Samsung Galaxy S7 kuwa imara na kutoweza kudukuliwa.
One Comment
Comments are closed.