Kampuni ya kijapani ya Sharp imetengeneza simu ambayo pia ni Roboti, ikiwa imepewa jina la Robohon simu hii inaumbo la roboti lakini inauwezo wa simu janja. Robohon inauwezo wa kupiga simu kutuma meseji lakini pia inafanya kazi nyingi za roboti.
Roboti hiyo ambayo imewekwa sokoni katika bei ya kuanzia na dola 1800 za kimarekani ambayo ni bei kubwa lakini ukiangalia mambo ambayo inayafanya unaweza kuona hiyo sio kubwa sana.
Roboti huyo anao uwezo wa kusoma meseji zako ambazo unatumiwa kwa sauti pindi zinapoingia ingawa sina uhakika kama mimi binafsi ningependa mtu kusoma meseji zangu kwanguvu mbele za watu lakini hii inawezakuwa ni huduma nzuri hasa kama ukiwa unafanya shughuri kama kupika na kufua.
Roboti huyu pia anaweza kutumika kama msaidizi wako ambaye anaweza kumwambia majukumu yako ya siku na yeye atakukumbusha pindi muda unapofikia. Pia roboti huyu anaweza kukusaidia kupiga picha nzuri.
Pengine moja ya kazi ambayo roboti hii inaweza kufanya na ambayo mimi binafsi nimeifurahia ni uwezo wake wa kufanya kazi ya projector na kurusha video ukutani zikiwa na picha bora kabisa.
Robohon anaendeshwa na Android 5.0 na anakuja na screen ya LCD ya nchi mbili (2″) ambayo ni ndogo sana kwa matumizi ya kawaida ya simu lakini pia simu hii ni kubwa sana kutosha katika mfuko hivyo bado ni changamoto kwa mmiliki kuweza kuibeba kwenda nayo mahala popote anapotaka.
Teknolojia inakuwa na wabunifu wanaleta mambo mapya, tuambie unaionaje roboti hii ambayo pia ni simu?