Teknolojia ya utengenezaji roboti wadogo na wakubwa wanaosaidia kazi mbalimbali kufanyika kuanzia viwandani hadi majumbani unazidi kukua. Ila roboti wote huwa wanaitaji kuchajiwa na mara nyingi inakuwa kwa kutumia umeme, leo mfahamu roboti mdogi anaye enda kwa jina la Row-bot asiyeitaji kuchajiwa kamwe.
Kuna watafiti mbalimbali duniani wanaojituma kwa nguvu kubwa kuja na teknolojia na vitu kama roboti ambavyo vinasaidia katika mambo ya kijamii badala ya kutengeneza bidhaa za kibiashara.
Muonekano wa Row-bot
Kwa kifupi roboti huyu – ‘kupitia bakteria spesheli walio ndani yake’ atakuwa anakula vijidudu vyote vyenye madhara na hivyo kusafisha maji hayo.
Row-bot imetengenezwa kuweza kuelea kwenye maji na wakati huo kuruhusu maji kuingia na kutoka ndani yake huku kikizunguka juu ya maji. Ndani yake kuna bakteria spesheli wenye uwezo wa kusafisha maji kwa kutafuna (digest) chembechembe chafu zilizo kwenye maji (pollutants).
Kinachozaliwa baada ya tukio hilo ni Carbon Dioxide na umeme, umeme huo unatumiwa na roboti huyo kuendelea kufanya kazi. Na hivyo kutoitaji umeme wa ziada kamwe.
Mchoro unaoonesha ubunifu ulioenda kwenye utengenezaji wa roboti huyo
Ugunduzi na utengenezaji wa teknolojia hii unaonekana unaweza kutumika katika maeneo mbalimbali ya uchafuzi wa mazingira unaohusisha maji – hii inaweza ikawa kwenye mabwawa, mito na labda ata bahari uko mbeleni.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Mbunifu na mpenda teknolojia.
Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM
Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.
| mhariri(at)teknokona.co.tz |
One Comment