Jambo la kutumia memori kadi kama njia mojawapo ya kuhifadhi data zetu kwenye simu, kompyuta limekuwa kitu cha kawaida sana kutokana na uwepo wa teknolojia ambayo kila siku mapya yanazidi kuvumbuliwa.
Kitendo cha mafaili kujificha na kuwa shida kuonekana limekuwa tatizo linalowasumbua watu wengi (hasa kwa wale wasiojua kutumia kompyuta kiundani) na kufanya watu kupoteza data mbalimbali ambazo hawakuzitunza sehemu nyingine yoyote mbali na kuzitunza kwenye memori kadi.
Njia za kufuata ili kuweza kurudisha mafaili ambayo yamejificha kwenye memori kadi.
Hapa ndipo kiini cha lengo la makala hii na ni muhimu kuwa na kompyuta ili kuweza kufanikiwa kurudisha zile data zako ambazo zilipotea tu bila hata ya wewe kuzifuta au kufutwa na mtu. Mara nyingi tatizo hili husababishwa na virusi ambavyo vipo kwenye memori kadi.
Fuata hatua zifuatazo kurudisha kumbukumbu kwenye kifaa chako (memori kadi):-
- Pakua “AutorunExterminator” kwenye kompyuta. Programu hii itasaidia kuondoa mafaili ya “autorun.inf” ambayo ni moja ya aina ya virusi. Bofya AutorunExterminator kuweza kuipakuwa programu hiyo.
Fungua (extract) kisha bonyeza AutorunExterminator kuweza kuinstall programu hiyo kwenye kompyuta. Baada ya AutorunExterminator kuwa kwenye kompyuta unganisha kifaa chako kwenye kompyuta.
- Kwenye keyboard ya kompyuta bofya Start (yenye nembo ya Windows) kisha andika Run. Ukurasa mpya utatokea kisha andika “cmd“.
- Andika “attrib -h -r -s /s /d g:\*.*” kwenye cmd (wenye rangi nyeusi). Herufi ya mwisho inabadilikana kulingana na kifaa chako kimepewa herufi gani kwenye kompyuta unayotumia. Inaweza kuwa herufi K, J, n.k. Kisha bonyeza Enter.
- Subiri kwa dakika kadhaa mpaka uone mchakato mzima umemalizika.
Zinaonekana ni hatua rahisi na chache za kufuata ili kuweza kurudisha mafaili yaliyokuwa yamepotea ila umakini mkubwa unatakiwa wakati unafanya jambo hili na kama hujiamini basi wasiliana nasi TeknoKona tutajua jinsi ya kukusaidia.
Chanzo: ccm.net
One Comment
Comments are closed.