Google kupitia chapa ya Pixel wametangaza saa yao janja inayojulikana kama Pixel Watch, saa hii inakua ni ya kwanza kabisa ambayo inatumia chapa hiyo.
Ni wazi kuwa soko la saa janja kwa sasa linakua kwa kasi kabisa na kutokana na ujio wa simu janja za Pixel 7 na Pixel 7 Pro kampuni imeona ni sawa kuleta na saa janja ya Pixel Watch katika soko.
Fitbit kampuni ambayo ilinunuliwa na Google hapo awali, itakua na teknolojia ndani ya saa janja hii, hata juzi juzi baadhi ya taarifa ambazo zilikua zinatumika Fitbit zilitakiwa kutumika zile za Google, Soma zaidi >>HAPA<<
Kingine kkizuri kwa saa janja hizi ni kwamba bado hazijakamilika kwa asilimia 100 katika swala zima la program endeshi maana wanasema kuna sasisho ambalo watalitoa ili kukamilika.
Vipengele hivyo ambavyo kwa sasa vinakosekana ni Blood Oxygen Tracking (kufutilia taarifa za kimwili kwa kutumia damu na oksjeni ya mwili), na Fall Detection features (kipengele cha kuhisi mtikisiko wa muanguko), ambavyo vitakuja kupatikana baadae kutokana na sasisho (update).
Soma sifa za saa janja hii >>HAPA<<
Kingine ni kwamba saa janja hizi zinaweza zikaanza kupatikana sokoni ikifika tarehe 13 ya mwezi wa 10 mwaka huu
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unaweza ukaanza kutumia saa janja hizi na ukaachana na zingine?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.