Njia ya ku’Hibernate’ inaonekana katika ‘Operating system’ (OS) kama za Windows na hata OSX (MacBook). Hii njia yaku Hibernate inakusaidia kuisimamisha kompyuta (laptop) yako katika hali iliyoko ili baadae ukija kuwasha uendelee pale pale.
Mfano kama ulikua unaandika kitu katika Microsoft Word ukiwasha laptop yako basi utaendelee hapo hapo ulipoishia (Microsoft word). Hard disk ndio inahifadhi hali ulioiacha wakati una hibernate laptop yako. Nilikua natumia njia hii ya ku hibernate laptop mpaka nilipokuja kujua hasara zake… lakini kwa nini usi hibernate laptop yako?
Katika Windows utaona kabisa sehemu imeandikwa ‘hibernate’ lakini katika OSX (Macbook) utaona imeandikwa au imepewa jina la ‘safe sleep’
‘HIBERNATE’ INAFANYA NINI HASA?
Hibernate inaitwa ‘usingizi mzito’ kwa laptop yako. Kwa ufupi njia ya ku’hibernate itagandisha hali ya kazi inayofanya katika RAM ya laptop yako na kisha kuipeleka katika HARD DISK na kisha laptop kuzimika. Hibernate inawasha mashine (laptop) tofauti na njia ya kawaida ya kuwasha na inachukua muda kwa mashine hiyo kuwaka tofauti na ukiwa katika ‘sleep mode’
KWA NINI TUSITUMIE NJIA YA KU’HIBERNATE?
Baada ya kujua hibernate ni nini na nini kinafanyika mpaka inatokea laptop ina hibernate, hizi ni sababu ambazo zinakushauri usipende kutumia njia kwenye kifaa chako (laptop).
Ku’hibernate laptop yako kutamaliza au kutatumia kiasi kikubwa cha betri pia kupunguza maisha ya betri la laptop yako. Pia ina athiri ‘system’ nzima ya ndani ya ndani ya mashine yako. Jiepushe na Njia hii lakini kama unatumia njia hii ya hibernate au sleep mode mara chache sana hiyo ni sawa maana njia hizi zimewekwa spesheli ili kutumika mara chache sana.
Sasa umejua kwa nini usiherbernate laptop yako?. Tumia njia yaku hibernate pale tuu inapobidi au jiepushe nayo ili kuongeza maisha ya laptop yako . Makosa kama ku’hibernate huku unaangalia muvi au huku kuna CD inayotumika katika laptop yanaweza kabisa kukuharibia mashine na hata hivyo itapata joto sana (kuchemka)
Inapokubidi kutumia ‘hibernate’ hakikisha unaweka laptop sehemu inayopata hewa vizuri. Hakikisha uifuniki au kuiweka kwenye begi au kuifunika kwa kitambaa au nguo ya aina yeyote.
Page ya Telegram hamuiupdate kwa Taarifa siku hizi kwa nini?
Asante Beatus, kuanzia leo tutaendelea kuiupdate kwa taarifa zaidi.