Apple ina vifaa vingi sana ambavyo kwa namna moja au nyingine vinaingizia kampuni pesa za kutosha moja wapo ni Apple Watch au wengine waniita iWatch.
Kumbuka Apple Watch sio kwamba ndio biashara yao kubwa kabisa kumbuka biashara kubwa kabisa ni iPhone ambayo inaingiza pato kubwa kuliko zingine.
Marekani wao wametoa katazo kwa saa hizo kuingia katika soko lao na sababu wameziweka wazi kabisa juu ya jambo hilo.
Katazo hilo ni kwa saa za Apple ambazo ni za kisasa zaidi –kumbuka kuna matoleo mapya na za nyuma—hivyo hata teknolojia haziwezi kuwa sawa kati ya saa hizo.
Apple imekatazwa kuuza Apple Watch ambazo zina mfumo na sensor za kupima kiasi cha Oxygen kwenye damu, imekatazwa kuuza Apple Watch za Series 9 na Ultra 2, kutokana na madai ya uvamizi wa hati miliki kwenye teknolojia ya kifaa cha kupima oksijeni ya damu katika saa za Apple Watch; imeiga na kuiba haki za kampuni ya Masimo.
Inaonekana Apple imeshindwa kesi yake dhidi ya Masimo kwa sababu kweli iliiba haki miliki ya Masimo katika mfumo wake wa saa za Apple Watch.
Ili Apple iweze kuuza saa zake, inapaswa kuzima mfumo wa kupima kiasi cha oksijenu (Oxygen) katika saa za Series 9 na Ultra 2. Hivyo kuanzia leo watumiaji wa Marekani ambao wananunua saa mpya hawatapata kipengele (feature) hii.——-Maneno Hayo Juu Ni Ya Sw.Tek
Je unadhani Apple itafanikiwa kuwa na mauzo mengi kwa saa hizi kama wakiendelea hivi hivi au inabidi wafanyeje ili kuhakikisha watumiaji wake wanapata kila kitu katika saa hizo?
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment juu ya maono yako kuhusiana na hili
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.