Kukaa karibu vifaa vyetu vya kielektroniki wakati tunaangalia vitu kama vile kutoka kwenye Tv ni hatari. Kumbuka hata wewe ulivyokuwa mdogo nna imani ulikua ukikatazwa kusogelea TV. Sasa basi Samsung wameliona hilo na kuja na ufumbuzi.
Sawa pengine labda kwa sasa inaweza ikawa ni vigumu kutazama Tv, najua watu wengi siku hizi wanakomaa kwenye simu na kompyuta kumbuka hata vioo hivyo vina mazara tuu pale unapo vikaribia.
Simu zetu watoto au wadogo zetu wanaweza wakawa wanazitumia kama vifaa vya kusababisha furaha yao, wanaweza wakaamua kucheza michezo mbali mbali na mda mwingine wanaweza wakatumia kama njia ya kusomea. Sasa utawezaje kuwaweka mbali na kioo cha kifaa wanachotumia
Shukrani kwa Samsung ambao wamekuja na App inayojulikana kama Safety Screen, hii inatumia teknolojia ya kugundua sura (facial recognition). App hii itagundua kama mtumiaji wa kifaa hicho yuko karibu na kioo cha kifaa.
Kama mtumiaji akiwa karibu na kioo basi kitatokea kikatuni, ambacho kitamjulisha mtumiaji kwamba yupo karibu na kioo cha kifaa na hivyo inabidi arudi nyuma. Endapo mtumiaji atakapoungeza umbali wa kutoka alipo na kifaa hicho basi hicho kikatuni kitaondoka, kumjulisha kwamba yupo umbali sahihi.
Samsung wametengeza App hii wakiwa na madhumuni mengi. Zuri kati ya madhuni hayo ni kwamba App hii itamjenga mtoto kujua njia nzuri ya umbali wa kutumia pale anapotumia vitu vya kielektroniki kama vile Tv.
Kumbuka kama mtu akiwa anatumia muda mwingi sana katika kuangalia kitu katika skrini ana hati hati ya kuharibu macho yake na hiyo ikiwemo kuharibu uwezo wake wa kuona kabisa.
Cha kufanya ni kupakua App hii katika kifaa chako na kuanza kuitumia. Utumiaji ni wa aina yake kwani mwenye kifaa anaweza kuiwasha na pia kulinda uwashaji huo na nenosiri. Yaani inamaanisha kama App hiyo ikiwashwa hakuna mtu anaeweza kuizima labda awe ni Yule mwenye nenosiri.
Tovuti Yao ni www.samsungsafetyscreen.com
Shusha App Hiyo Hapa – Android