Ndiyo watu wengi wanapenda kuongeza uzuri wa picha zao kwa utundu wa kubadilisha rangi na mtazamo mzima. Lakini pia si kila mtu anataka ajiunge Instagram ili aweze fanya hivyo.
Zifuatazo ni baadhi ya Apps bora kabisa zitakazokuwezesha kubadili muonekano wa picha zako (‘effects’), na zaidi ya yote nyingi zina uwezo mkubwa katika suala hili kuzidi ata Instagram.
Kila baada ya maelezo nimekuwekea sehemu ya kubofya itakayokupeleka kwenye duka la Google Play ili uweze kushusha (download) na kuweza kupakua app hiyo kwenye simu yako. Kumbuka hizi zote ni za bure kabisa.
1. Pixlr-o-matic
Nimeijaribu app hii kwa kweli ipo poa sana. Ina uchaguzi mwingi sana wa mabadiliko ya mtazamo (effects), baada ya kuchagua na kuongeza unaweza kuzituma kwenda kwenye apps zako nyingine kama Facebook, Whatsapp, Instagram na kwingineko.
Kuipakua Kuiweka Kwenye Simu yako Bofya Hapa!
2. PicFrame
Ni moja ya app maarufu kwa wengi. Hii itakuwezesha sio kubadilisha muonekano wa rangi pekee bali pia utaweza kupanga picha mbalimbali kwenye mpangilio mmoja unaoupenda mwenyewe kama wa drafti na nyinginezo.
Kuipakua Kwenye Simu yako Bofya Hapa!
3. PicSay
Hii ni app nzuri zaidi pale utakaotaka kuwa unataka kuleta uchekeshi au kuongeza njonjo zingine za kawaida kwenye picha. PicSay inakuwezesha kuongeza maneno na vitu vingine kwenye hiyo picha.
Kuipakua Kwenye Simu yako Bofya Hapa!
Hizi ni baadhi tuu, je wajua app gani ambayo pia unafikiri inastahili kukumbukwa?
No Comment! Be the first one.