Siku chache zilizopita niliandika juu ya sakata la simu za Android kuhusishwa na utumwaji wa barua pepe za SPAM baada ya kuathiriwa na kutumiwa na vijidudu flani vya elecktronik maarufu kwa mfumo wa BOTNET.
Kwa habari za sasa ni kwamba lawama si kwa programu ya Android ila ni kwa mtumiaji mwenyewe. Ni kweli Android kama Syambian, iOS na Windows nayo pia inaweza athirika na BOTNETS ila mtumiaji ndiye mwenye usukani mkuu.
Je ni wapi unatumia kupata apps za simu/tablet yako? Kama unashusha (download) apps za Android kutoka kwenye Soko la Apps salama kama Google Play upo katika usalama wa kutokutwa na janga hili. Lakini kwa wale wanaoshusha apps kutoka mitandao isiyoaminika kuna uwezekano mkubwa sana wa simu yako kuwa muathirika wa BOTNETS.
Watafiti wamegundua zaidi ya asilimia 90 ya simu zilizoathiriwa na BOTNETS ni zile kwenye nchi zinazoendelea na hii inachangiwa kutokana na wengi wetu kukimbia masoko ya App kama Google Play kutokana na kutaka apps ambazo huwa zinapatikana kwa kuuzwa hivyo tunaenda kutafuta za bure kwenye mitandao isiyorasmi.
Hivyo kama unatumia app za huduma za barua pepe hasa ya Yahoo Mail kwenye simu yako ya Android kuwa mwangalifu sana kwani simu/tablet hiyo ikiathiriwa na BOTNETS itakuwa inatuma barua pepe za SPAM kwa watu mbalimbali bila idhini yako wala kukupa taarifa hiyo.
No Comment! Be the first one.