Moja ya kompyuta ambayo imeleta mapinduzi makubwa katika maswala mazima ya teknolojia ya komyputa na ilikua ikimilikiwa na Steve Jobs, yule wa Apple inapigwa mnada.
Ngoja kwanza! kwa sasa sio kompyuta kamili (Kwa mfano Apple 1 yote), kwa sasa ni sakiti tuu au kwa kimombo wanasema ni Printed Circuit Board (PCB).

Sakiti hii inatgemewa kukuza walau dola 500,000 za kimarekani, kumbuka kompyuta nyingi sana za Apple ambazo zilitokana na sakiti hiyo zimekua zikifanyiwa minada sana hivi karibuni, hapa nayaongelea matoleo ya Apple- 1 zile za miaka ya 1976.

Kumbuka pia sakiti hii ya kwanza kabisa ambayo ilikua inamilikiwa na marehemu Steve Jobs ndio ambayo imefanya mpaka kutengenezeka kwa kompyuta hizo za mwanzo kabisa kutoka Apple.
Kingine watu wasichokijua ni kwamba sakiti hii ya ndio ilitumika na Steve Jobs kumuonyesha mfanya biashara Paul Terrell, nae akakubali kununua kompyuta 50 kutoka kwa Steve Jobs lakini kulikua na sharti.

Na sharti ni moja tuu manunuzi hayo yangekamilika kama bwana Steve angeweza kuzitafutia mifuniko sakiti hizo—ndipo angempeleke 50 – hii ikamfanya bwana Paul Terrell kuwa wakwanza kuanza kuuza kompyuta hizo kwa reja reja.

Mnada huu wa sakiti hiyo ya Apple 1 unategemewa kumalizika kabisa mwishoni mwa mwezi agosti, kingine kinachoweza kupelekea sakiti hii ikauzika kwa bei kubwa sana ni sababu iko moja tuu (ambayo ni ya kwanza).
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unaweza kuwa tayari kabisa kununua na kumiliki vitu vya aina hii katika mnada?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.