Samsung Galaxy A51 imekuwa simu janja ya kwanza kufanana na iPhone na hii imefanya rununu (Galaxy A51) kuwa na upekee wa aina yake. Je, unajua ni upi huo?
Ukichukua simu janja Samsung Galaxy A51 na iPhone nyingi tuu ambazo ni za miaka ya karibuni utatambua kuwa rununu hizo zinafanana kwa kitu ambacho kinaifanya simu janja tajwa inayotumia Android kuwa ni ya kipekee. Upekee wa simu hii unatokanana na kwamba kuwa ndio rununu ya kwanza kuwa na sehemu ya kuchomeka chaji (lightning port) iliyo katika teknolojia ya juu.
Yuleyule aliyezifanya iPhone nyingi za mwaka zikawa na USB-C ndio huyo huyo ameipeleka teknolojia hiyo kwenye Samsung Galaxy A51 na kuifanya kuwa simu janja ya kwanza inayotumia Android kuwa na sehemu ya kuchaji/kuleta mawasiliano kati ya simu na kompyuta kwa teknolojia ya kisasa zaidi.

Kama utakumbuka vyema Umoja wa Ulaya unataka kuwa simu janja zote ziwe zinatumia kimemeshi cha aina moja kwani haipedezi kuwepo na “Takataka” nyingi bila sababu kutokana na kwamba mtu akinnunua rununu nyingine na kama chaji haziingiliani basi ile ya zamani inakuwa haina kazi tena.
Je, huu ndio mwanzo tuu wa kuzifanya simu janja ziwe zinatumia chaji ya aina moja? Kazi yetu ni kusubiri kuona kama makampuni yatakubali kubadilika bila shuruti.
Vyanzo: Pro Pakistan, GSMArena
No Comment! Be the first one.