Samsung ni moja kati ya makampuni ya kiteknolojia ambayo inajihusisha na vitu vingi sana lakini kwa haraka haraka inafahamika kuhusiana na simu janja zake tuu.
Ni wazi kwamba kampuni inatengeneza na kuuza mpaka majokofu, Tv, Laptop na vitu vingine vingi tuu.
Kingine ni kwamba kwa sasa kampuni ina miaka kadhaa nyuma tangu iingine katika soko la kuuza na kutengeneza kompyuta mpakato (laptop) na sasa ina mpango wa kutoa toleo lingine la Galaxy Book.
Toleo hilo litakua limeboreshwa zaidi ukilinganisha na toleo la nyuma na uboroshwaji huo utajikita katika muonekano na hata ufanisi wake kwa sababu utakua na sifa bora zaidi kulinganisha na ile ya nyuma.
Kingine ambacho watu wengi hawakutegemea ni kwamba kampuni ya Samsung yenyewe imesema kwamba itatangaza laptop hiyo mpya sambamba na Samsung galaxy s23.
Tukio hilo la utangazaji wa bidhaa hizo mbili zinategemewa kutangazwa katika tukio hilo la Samsung mwaka 2023
Tukio ambalo linakwend akwa jina la Samsung Unpacked 2023 event ambalo pengine linaweza kufanyika February moja.
Kingine ni kwamba tukio hili linaweza likawa refu sana ukilinganisha na matokio mengine ya Samsung ambayo yamewahi fanyika.
Kitu ambacho kitasababisha hili ni kwamba kampuni ina mpango wa kutambulisha vifaa vingi sana kwa pamoja ukilinganisha na kipindi cha chini.
Kwa sasa hakuna sifa za uwazi kabisa za laptop hiyo maana bado kampuni haijaweka wazi—siku ya tukio mambo yote yatakua hadharani.
Galaxy book ni laptop kutoka Samsung zenye umbo dogo lakini zinakua na sifa za juu kabisa na kwa haraka haraka toleo jipya linadhaniwa kwa kiasi kikubwa cha uboreshwaji wa muonekano na ufanisi kama nilivyosema.
Je unadhani ni kitu gani kinaweza kikawa kimeongezeka ukilinganisha na ile ya zamani, ningpenda kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.