Miaka na miaka Samsung wamekuwa wakitoa simu ambazo zinakuwa na programu endeshi inayotumiwa na wengi lakini safari hii huenda mambo yakawa tofauti kidogo kwa kuleta simu yao ya kwanza iliyo na Android Go.
Samsung ambao inasemekana kwamba wanategemea kutoa simu yao ya kwanza kabisa ikiwa inakluja ikiwa na toleo la programu endeshi iitwayo Android Go huku simu hiyo ikiwa tayari imeshapewa jina; Samsung J2 Core.
Je, Sansung J2 Core ina sifa gani?
Kiujumla sio simu janja ambayo unaweza ukaitumia kufanya kazi nzito; ni simu ambayo haitaweza kufanya zile kazi nzito mathalani kucheza magemu mazito, kuangalia sinema kupitia kwenye simu hiyo, n.k. Hii ni kwa sababu zifuatatazo:-
RAM/Memori ya ndani. Samsung J2 Core inaaminika kuwa itakuwa na RAM ya GB 1 huku memori yake ya ndani ikia na uwezo wa kuhifadhi vitu vya mpaka GB 16 tuu.
Prosesa. Hapa kwa mujibu wa fununu ni kwamaba simu hiyo itakuwa na kipuri kiitwacho Exynos 7570 huku kasi yake ikiwa ni 1.4GHz pekee. Kwa kasi hii ya prosesa haishauriwi kabisa kuweka programu nzito.
Kamera. Ingawa simu hiyo imeangazia wale watu wenye matumizi ya kawaida kwenye simu lakini kitu kizuri ni huenda ikawa na kamera mbili; kamera ya mbele itakuwa na MP 5 huku ile ya nyuma ikiwa na MP 8.
Betri. Betri ya kiwango cha 2600mAh kwa hakika ni ya kawaida sana ambayo iwapo utaitumia kwa kazi nzito basi tegemea kuichaji kila mara baada ya saa chache kupita.
Inawezekana una mtoto, ndugu, rafiki au hata mzazi ambae hajawahi kabisa kutumia simu janja na sio mtu wa kupenda kufanya mambo mengi kwenye simu, basi simu kama hii pengine ikamsaidia sana.
Vyanzo: The Verge, Digital Trends