Teknolojia ya rununu (simu janja) ambazo zinaweza kujikunja/kujikunjua zinaonekana kurudi katika ulimwengu wa sasa wenye ushindani unaovutana kila uchwao. Samsung wanataka kuleta bidhaa ambayo inafana na ile ambayo waliizindua miezi kadhaa iliyopita ingawa itakayokuja itakuwa inafungnuka kwa nje.
Ulishasoma kupitia tovuti mbalimbali kuhusu Samsung Galaxy Fold na hata kufikia hatua ya kuzinduliwa ingawa hadi sasa haijaweza kupelekwa sokoni ili kuweza kununuliwa kutokana na matatizo ambayo yalibainika kwenye simu hiyo kitu kilichosababisha kuhairishwa mpaka hapo kasoro zote zilizobainika zitakapoondolewa.
Wakati tukiwa tunasuburia Samsung Galaxy kuingia sokoni fahamu ya kuwa kampuni hiyo inafanya mpango wa kuleta simu janja inayofunguka kwa nje huku ikionekana kuwa kinyume cha Galaxy Fold ambayo inatarajiwa kuja kabla ya Huawei Mate X itakayouwa inafunguka kwa nje sawa na ya mpinzani wake.
Toleo hilo jipya la simu inayojikunja/kujikunnjua huenda ikatoka mwezi Agosti 2019 kabla ya Huawei Mate X toleo jipya (inayofunguka kwa nje+inatumia 5G) kutoka mwezi Septemba ambao nao wameshindwa kutoa simu yao inayojikunja na kujikunja kutokana na matatizo ya kiufundi yaliyojitokeza kwenye rununu husika lakini pia changamoto ambazo Huawei wanapitia kwa sasa.
Hakuna undani zaidi unaofahamika kuhusu toleo jipya la Samsung Galaxy Fold lakini kuna taarifa kuwa kampuni husika wataendelea kutoa msururu wa simu za aina hiyo mpaka kufika mapema mwakani (2020). Kuweza kufahamu mengi zaidi unaweza ukaangalia picha jongefu hapo chini.
Vyanzo: GSMArena, Youtube