Walikuwa ni moja ya wapinzani wakubwa sana tokea lawama na kesi kubwa za madai kuanzishwa na Apple dhidi ya kampuni ya Samsung, haya yote yanaisha na sasa wapo tayari kushirikiana kibiashara.
Katika mkataba mpya baina ya kampuni hizi mbili kampuni ya Samsung kupitia biashara yake ya vifaa vya kielektroniki watakuwa wanatengeneza vioo vya kutumika katika simu na tableti zijazo za Apple na pia watahusika kutengeneza kadi ndogo (diski uhifadhi/ memory chips) zinazotumika katika simu na tableti hizo (iPhone na iPad).
Mahusiano baina ya makampuni haya yalianza kurudi kutokana na juhudi za mkurugenzi wa sasa wa kampuni ya Apple, Bwana Tim Cook ambaye mwaka jana mwezi wa nane alikubali kuanza kwa mazungumzo na kukubaliana kumaliza kesi na migongano iliyokuwa inaihusisha kampuni hizo mbili.
Kwa sasa Samsung watahusika katika utengenezaji wa kadi ndogo janja zitazotumika katika toleo lijalo la simu ya iPhone, pia watahusika na utengenezaji wa vioo (display) vya simu na bidhaa zingine zijazo kwa ajili ya kampuni ya Apple. Inasemekana tayari kampuni ya Samsung imeweka bajeti ya dhaidi ya Dola bilioni 14 za kimarekani (Kwa sasa Dola 1 ni takribani elfu 2 ya TZ) kwa ajili ya kukuza viwanda vyake viweze kukizi hitaji kubwa kutoka kampuni ya Apple.
Kama ulikuwa ufahamu bado ni kuwa kampuni ya Samsung ni moja ya makampuni yenye biashara nyingi zaidi duniani na huwa inahuzia makampuni mengine vifaa mbalimbali vya kielektroniki vinavyoitajika katika utengenezaji wa simu, tableti na vifaa vingine vingi vya kielektroniki.
Makubaliano haya ya kibiashara baina ya Samsung na Apple tayari yameleta habari mbaya kwa makampuni mengine ya barani Asia yaliyokuwa yanategemea biashara ya Apple. Makampuni mengine yanayofanya biashara hiyo ya kutengeneza ‘chips’ za elektroniki kama vile SanDisk (Kampuni kubwa ya utengenezaji wa diski uhifadhi/memory disks) tayari wamepunguza mahesabu ya faida na ukuaji wa biashara yao kwani walikuwa wanategemea zaidi kuiuzia Apple bidhaa zake.
Je ulikuwa unafahamu ya kwamba Samsung wanauwezo mkubwa sana kiteknolojia zaidi ya kutengeneza na kuuza simu tuu? Basi sasa fahamu ya kwamba atakama utanunua simu ya iPhone basi ujue vitu vingi ndani ya simu hizo vinanunuliwa kutoka kwenye makampuni mbalimbali.
No Comment! Be the first one.