Ni wazi kuwa toleo la Galaxy Z Flip 4 ni moja kati ya matolea ya simu janja za kujikunja yanyofanya vizuri sana katika soko kwa sasa.
Samsung iliweka wazi lengo lake la kuja na simu janja ya Galaxy Z Flip 4 ambayo ni spesheli ukilinganisha na ile ya kawaida ambayo imezoeleka na hapa wanashirikiana na Maison Margiela katika kuliwezesha hili.
Soko ambalo limekusudiwa kwa haraka haraka ni Korea ya kusini ambapo simu hiyo itazinduliwa ifikapo desemba 1.
Kingine ni kwamba toleo hili litapatikana kwa uchache sana maana kampuni ina mpango wa kuuza simu hizo zipatazo 100 tuu.
Ili kupata simu hii itabidi wateja waweza kuweka oda zao kupitia mtandao wa Samsung ifikapo tarehe moja na wale wateja wenye bahati wataweza kushinda –katika uchaguzi—na kisha watatumiwa simu zao.
Ukaichana na manunuzi hayo tuu simu hii ya kujikunja itakua ikionyeshwa katika baadhi ya stoo na kumbi kama vile stoo kubwa za Daechi, Gangnam, Hongdae, Lotte Department, Myeongdong, na sehemu kama vile……
……. Samsung Digital Plaza, bila kusahau stoo ya The Hyundai Seoul Maison Margiela nah ii itafanyika kuanzia tarehe 25 novemba mpaka kufikia disemba 2.
Maison Margiela ni chapa kubwa sana na inatengeneza vitu mbalimbali kama vile mavazi n.k na kwa sasa chapa hiyo inatoa toleo lake la Samsung Galaxy Z Flip 4.
Sio mara ya kwanza kwa chapa za simu kutoa matoleo ya simu ambayo yako spesheli kwa dhima Fulani ukiachana na kawaida ya chapa hiyo.
Toleo hili halitakua na utofauti mkubwa katika sifa za undani ukilinganisha na toleo lile la kawaida la Galaxy Z Flip 4 lakini utofuti wa kimuonekano utakuwepo
Utofauti huo ni kwamba simu itakua na chapa kadha wa kadha za Maison Margiela. Upande wake wa nyuma una mchoro ambao unafanana na jinsi ndani simu ilivyo.
Mfumo wake wa uendeshi (Software) una mabadiliko kidogo tena ni yale ya kimuonekano tuu. Simu hiyo inakuja na kava la ngozi nyepesi (leather) huku likiwa na kichuma cha kushikilia simu isinguke vile vile likiwa na namba 11 kw anyuma kama utambulisho wa chapa ya Maison Margiela.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unaweza nunua kifaa cha kieletronikia ambacho kimetolewa spesheli na chenye upatikanaji mchache?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.