Kwa wale mashabiki wa ubishi wa bidhaa za Apple au Samsung, kwamba ipi ni bora zaidi, ubishi umetiwa chachu tena kwa mara nyingine, kwani Samsung wametangaza Galaxy Tab S2, tabiti zinazofuta rekodi za u-wembamba uliowekwa kwanza na iPad Air 2 ikifuatiwa na Sony Xperia Z4 Tablet na Dell Venue 8 7000.
Tabiti hizo mpya ziko za aina mbili na zote zinakuja na fremu ya chuma yenye upana wa milimita 5.6 (nusu sentimita), ambayo ni ndogo zaidi ya rekodi ya milimita 6.1 iliyowekwa na Apple, Sony na Dell.
Kama ilivyokuwa kwa iPad zilizotolewa mwaka uliopita na simu kadhaa mpya, tabiti hizi mpya za Samsung zinakuja na teknolojia ya ku-’scan’ alama za vidole (‘integrated fingerprint scannes’).
Ukilinganisha na tabiti za Galaxy ya mwaka jana (Galaxy Tab S 10.5 na 8.4), tabiti mpya za Samsung zina vioo vidogo zaidi (inchi 9.7 kwa kubwa na inchi nane kwa ndogo) ila zina uzito mdogo zaidi (gramu 389 na 265), zaidi ya tabiti za aina yake duniani.
Tabiti hizi zinaendeshwa na Android Lollipop 5.0 na zina kioo cha aina ya Super AMOLED (20148x1536p resolution kama ya iPad Air 2).
Sifa Zaidi:
- Prosesa: 64-bit octa-core Samsung Exynos 7420 (quad-core processors mbili)
- Kumbukumbu (RAM): GB 3
- MicroSD: Ukubwa hadi GB 128.
- Uhifadhi wa ndani: GB 32 and GB 64.
- Kamera: MP 8 nyuma na MP 2.1 mbele.
Akizungumzia katika tukio la kutangaza Tab 2, JK Shin, mkurugenzi na rais wa kitengo cha IT na Mobile cha Samsung Electronics, alisema, “Pamoja na kuwa Galaxy Tab S2 ni tabiti nyembamba zaidi tulioweza kutengeneza, inawapa watumiaji uwezo haraka na kirahisi wa kuona vitu vingi vya kusaidia kufanikisha ufanyaji kazi.” Kampuni hiyo ya Korea imetangaza kuwa tabiti hizo zitaweza kupatikana mwezi wa Agosti na kuendelea, kwa bei ya kuanzia Euro 399 (Tsh. 931, 641).
Je, unajisikiaje kuhusu habari hii. Tuungane kwenye mazungumzo hapo chini.
Picha: samsungtomorrow.com, sammobile, trustedreviews, tablet-news
No Comment! Be the first one.