Kupitia kitengo chao cha utafiti wa kiteknolojia kampuni ya Samsung imekuja na teknolojia inayoweza kusaidia kwa kiasi kikubwa utokeaji wa ajali zinazohusisha watu kutaka kuyapita malori (ku-overtake). Ajali nyingi katika nchi zinazoendelea huwa zinatokea katika ku-overtake malori malefu bila kuona vizuri kinachokuja kwa mbele.
Teknolojia hii inahusisha utumiaji wa kamera spesheli zilizopo mbele ya roli na kuonesha kupitia TV kubwa inayokuwa sehemu ya nyuma ya lori. Wamedai TV hiyo iliyotengenezwa spesheli ina vioo spesheli za kuifanya iwe salama dhidi ya uvunjikaji wa kirahisi, pia kamera hizo zitaweza kuonesha vizuri ata wakati wa usiku.
Waandishi wengi wametoa sifa kwa kampuni hiyo kwa wazo hili la kitofauti. Samsung wanasema teknolojia hii itaweza kusaidia ajali za aina mbalimbali, kama vile kujua gari linalokuja kabla ya kufanya maamuzi ya ku-overtake.. pia ajali zinazotokana na malori kufunga breki za ghafla kutokana na wanyama au watu kuvuka barabara ghafla.
Kwa sasa Samsung wamefanikiwa kufanya majaribio ya teknolojia hiyo nchini Argentina ambayo ni moja ya nchi zinazoongoza kwa ajali za malori na hadi sasa wengi wameisifia sana teknolojia hiyo. Kilichobaki kwa sasa majaribio zaidi na wao kufanya maboresho na kisha kuomba kibali rasmi katika nchi mbalimbali ilikuweza kupata baraka ya utumiaji wa teknolojia hiyo.
Malori hayo wenyewe wameyapa jina la ‘Samsung Safety Truck’.
No Comment! Be the first one.