Ukiachana na vitu vingi ambavyo kampuni ya Samsung inasifika kutengeneza kama vile simu na TV bado kampuni inatengeza vioo vya vifaa mbalimbali.
Kwa upande wa Samsung ukizungumzia vioo vya kujikuja (Foldable) katika simu tayari wameshaliteka soko hilo maana wana simu kali sana zinazotumia teknolojia hii.

Habari hii imewafikia wengi baada ya Samsung wenyewe kutoa ripoti yake ambayo ina malengo ya kampuni katika upande wa uzalishaji.
Lakini ni wazi kwamba Teknolojia hii ilikua ikisubiriwa kwa hamu sana na watumiaji na pia hata ukiangalia ni kwamba kuna makampuni mengi yanafanya mpango yawe na teknolojia kama hii.
HP nao wako katika hatua za maandalizi kabisa katika kuhakikisha wanakuja na Laptop yenye kioo cha kukunjika (Foldable) kwa kupitia ushira wake na LG.
Vyanzo vingi mpaka sasa vinasema Samsung ndio ambao wamepiga hatua zaidi katika teknolojia hii na unaweza usishangae kwamba Laptop ya kwanza kabisa kutumia teknolojia hii ikatokea kwao.

Asus ZenBook 17 Fold ni lapatop ambayo nayo ilikuja na teknolojia hii lakini haikufanya vizuri sana katika soko na vile vile ilikua ni moja kati ya Laptop zenye Gharama.
Ila kwa teknolojia ya aina hii ni kawaida sana kwa vifaa kuwa na gharama za juu kutokana na gharama za uzalishaji hili lilionekana hata katika simu za Samsung Fold.
Kingine ni kwamba usije ukashangaa Samsung wakawa wanawatengenezea vioo hivyo vya kujikunja kwa makampuni mengine (kwa mauziano) maani ni moja kati ya mfanyaji biashara mzuri wa vipuri.

Mpaka sasa Samsung ndio mzalishaji mkubwa wa vioo vya OLED duniani kote na amekua akitengenezea makampuni mengi vioo mfano vioo kwa Apple kwenye baadhi ya iPhone 14.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hili umelipokeaje? Je unadhani Laptop hiyo itakua ni ya bei ya juu sana?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.