Samsung kampuni nguli kabisa katika teknolojia za kurahisisha mawasiliano imetangaza tabiti mpya — Galaxy Tab Active 4 Pro — ambayo inakuja mahususi kwa kundi la watu.
Tabiti hii– Galaxy Tab Active 4 Pro ni mahususi kwa wafanya kazi na hata wale ambao wanafanyakazi nzito maana inakuja katika hali ya uimara sana ukilinganisha na tabiti zingine kutoka kwao Samsung.
Wafanyakazi kama wale wa viwandani, migodini, wataalam wa hospitalini n.k tabiti hii inawafaa sana maana inakuja na programu kadha wa kadha ndani yake ambazo zina sifa kabisa za kuendana na zile za ofisini.
Kingine kizuri ni kwamba program hizo utakua na uwezo wa kuzibadilisha badilisha na kuziweka kuendana na mazingira ya kazi ambayo ipo.
Ukiachana na muonekano wa tabiti hii kua wa aina yake, Tabiti hii inakuja na baadhi ya sifa za undani zifuatazo:
Galaxy Tab Active 4 Pro | ||
Kioo (Display) | 10.1″ (255.4mm), 1920 x 1200 (WUXGA), TFT, 16M | |
Mfumo | Android | |
Ukubwa Wa Kioo | 170.2 x 242.9 x 10.2mm (674g) | |
Kamera | Kamera Ya Mbele | 13MP AF Flash |
Kamera Ya Selfie | 8MP | |
Video | UHD 4K (3840 x 2160)@30fps | |
Ujazo Uhifadhi | 4 + 64GB, microSD mpaka kufikia 1TB** | |
Prosesa | 2.4GHz, 1.6GHz Octa-Core Processor | |
Betri | 7,600mAh | |
Namna Ya Kutoa Loki (Lock) | Utambuzi Wa Sura, Alama Za Vidole |
Kwa haraka haraka ni kwamba kwa muonekano huu inamana tabiti hii itaepuka adha ya kupasuka pasuka kwa urahisi maana ina jumba imara ambalo linatoa ulinzi kuhusiana na jambo hilo.
Kuna tabiti nyingi kwa sasa, na ni mara chache sana makampuni kutoka tabiti mahususi kabisa kwa jambo moja, wengi wanaamini wanapunguza wigo wa soko lao. Kwa hili samsung wanahitaji hongera.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niambie je unaweza kuanza kutumia tabiti kama hii kwa maisha ya kawaida tuu kama sio mfanya kazi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.